Nahodha wa England, Harry Kane, amekiri kuwa tuzo ya Ballon d’Or ipo kwenye mawazo yake, akisema kila mchezaji wa soka anatamani siku moja kutambuliwa kuwa bora zaidi duniani. Kauli hiyo ya Kane imekuja siku moja baada ya kuandika historia nyingine akiwa na England. Mshambuliaji huyo alisherehekea mechi yake ya 125 kwa kufunga mabao mawili katika ushindi wa 3-0 dhidi ya Czech Republic, akifikia idadi sawa ya mechi za kimataifa na Peter Shilton.

Kane sasa ni miongoni mwa wachezaji wanaotajwa kuwa na nafasi kubwa ya kushinda Ballon d’Or baadaye mwezi huu, baada ya kuwa na msimu bora zaidi wa maisha yake ya soka akiwa Bayern Munich. Katika msimu uliopita, Kane alifunga mabao 61 katika michezo 51 na kusaidia Bayern Munich kutwaa mataji matatu ya ndani. Pia aliisaidia England kumaliza katika nafasi ya tatu kwenye Kombe la Dunia 2026.
Akizungumzia tuzo hiyo maarufu zaidi kwa mchezaji mmoja, Kane hakuficha tamaa yake ya kutaka kutambuliwa kama bora duniani. “Naamini kila mchezaji anataka kuwa mchezaji bora duniani. Ni moja ya mambo yanayokupa furaha kubwa unapopata kutambuliwa kupitia tuzo hizo,” alisema Kane.

Licha ya mafanikio hayo makubwa, Kane haamini kwamba amefikia kilele cha uwezo wake. Mshambuliaji huyo mwenye miaka 33 anaamini bado ana nafasi ya kuboresha kiwango chake na kuongeza mafanikio zaidi.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Alipoulizwa kama ameshafikia mwisho wa uwezo wake baada ya msimu wa kuvutia, alitoa jibu fupi lakini lenye ujumbe mkubwa: “Natumaini bado sijafika. Natumaini bado kuna mengi zaidi mbele yangu.”

Kwa sasa, macho yake yanaelekezwa kwenye Ballon d’Or, huku msimu wake wa kuvutia, mabao mengi na mafanikio ya Bayern Munich yakimfanya kuwa mmoja wa wanaowania tuzo hiyo kwa nguvu. Iwapo ataibeba, itakuwa mafanikio mengine makubwa katika safari ya nahodha huyo wa England.


