Nahodha na mshambuliaji wa timu ya taifa ya Uingereza Harry Kane amemtakia kheri gwiji wa soka wa Brazil Pele aweze kupona haraka kwa ugonjwa wake unaomsumbua.
Taarifa kutoka nchini Brazil zinaeleza kua gwiji huyo yupo kwenye hali mbaya zaidi baada ya tatizo lake la saratani kufika hatua mbaya na kushindwa kutibika tena hivo mpaka sasa anapewa uangalizi maalumu lakini hakuna tiba tena.Nahodha wa Uingereza Harry Kane wakati akiongea na waandishi wa habari leo alionesha kulipa fadhila na kukumbuka gwiji huyo alipomuongelea mwaka 2014 wakati akiwa na miaka 21 na kusema mshambualiji huyo ni kipaji bora kinachohitajika tu kujitunza tu ili aendele kua bora.
Kane akikumbuka maneno hayo alisema “Kwanza kabisa tunatuma salamu zetu za kheri kwake na familia yake, Sio mimi tu na kikosi kizima cha Uingereza. Yeye ni kioo kwenye mchezo wetu, mwanasoka wa ajabu na mtu wa ajabu hivo kusikia maneno kama yale kutoka kwake ilikua kitu cha kipekee sana. Inasikitisha kusikia habari kama hizo tunamtakia kheri mimi na wachezaji wenzangu wote wa Uingereza”Gwiji Pele ambaye amewahi kushinda ubingwa wa kombe la dunia akiwa na miaka 17 tu mwaka 1958 na kufanikiwa kuisaidia kubeba kombe hilo mwaka 1962 na 1970. Inaelezwa gwiji huyo yupo kwenye hali mbaya sana kiafya kwasasa na dunia nzima ya wapenda mpira ipo kwenye maombi kumuombea gwiji hiyo.