Kane: Kukosa Penati Kombe la Dunia Kumenipa Njaa ya Mataji

Mshambuliaji wa klabu ya Tottenham Harry Kane amesema kukosa penati dhidi ya Ufaransa kwenye michuano ya kombe la dunia imempa jaa ya mataji zaidi.

Mshambuliaji huyo ambaye alikosa mkwaju w penati dhidi ya timu ya taifa ya Ufaransa  hatua ya robo fainali kwenye michuano ya kombe la dunia nchini Qatar. Penati ambayo ingeiwezesha timu ya taifa ya Uingereza kusawazisha matokeo na kua mabao mawili kwa mawili.kaneHarry Kane ameshafunga mabao matatu ya ligi kuu ya Uingereza tangu kurejea kwa ligi baada ya mapumziko ya kombe la dunia, Huku akionekana kusahau uchungu wa kukosa mkwaju wa penati kwenye kombe la dunia na baada ya kurudi kwa kasi kwenye klabu yake.

Mshambuliaji huyo amekiri kua tukio la kukosa penati bado linamuumiza japo anaona ni sehemu ya mpira, Lakini pia anasema anaitumia kama changamoto kwenye kuhakikisha anafanya vizuri zaidi siku za mbeleni.kaneMshambuliaji Kane anaeleza ana furaha kwasasa kutokana na kiwango chake anachokionesha ndani ya klabu yake ya Tottenham, Pia anasema ana kazi kubwa ya kufanya hapo mbeleni kwajili ya kuhakikisha anashinda mataji na klabu hiyo.

Acha ujumbe