Kocha wa Chelsea, Thomas Tuchel amethibitisha kuwa N’Golo Kante alikosa mchezo dhidi ya Arsenal siku ya Jumatano usiku kutokana na maumivu ya Achilles. Lakini atakuwa fiti kuanza katika fainali ya FA hapo kesho.

 

kante, Kante Fiti Kuivaa Leicester Fainali ya FA., Meridianbet

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari kabla ya mchezo wa kesho :

“Tulichukua maamuzi pamoja, N’Golo, mimi na timu ya madaktari, kumpumzisha katika mchezo dhidi ya Arsenal kufanya matibabu ya Achilles katika mguu wa kulia, nadhani.” alianza Thomas Tuchel

“Ni kwaajili ya kuzuia maumivu, si jeraha kubwa, si la kuogopa kuwa litakuwa kubwa. Lilikuwepo na nililikuwa ninamsumbua.

“Amefanya mazoezi yote jana na leo, hakuna malalamiko yoyote. Ataanza katika mchezo wa kesho na tunategemea atamaliza mchezo pia.” aliongeza Tuchel.

Kante amekuwa mchezaji bora wa Chelsea FC hadi sasa msimu huu, na mchezaji huyo wa miaka 30 ametoa pasi mbili za magoli katika michezo 29 ya Ligi msimu huu.


PESA IPO HAPA KATIKA KASINO YA LUCKY LUCKY.

Hii ndiyo burudani yenye ushindi! Ingia kwenye kasino ya Meridianbet kufukuzia ushindi huu. Cheza sasa Lucky Lucky na uwe moja ya washindi na Mabingwa.

kante, Kante Fiti Kuivaa Leicester Fainali ya FA., Meridianbet

CHEZA HAPA

19 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa