Kante na familia yake walikimbia nchini Mali na kuingia Ufaransa katika harakati za utafutaji lakini kwa wakati huo mambo hayakuwa mazuri sana kwao. Alipoanza maisha ya shuleni alipenda sana kucheza mpira wa rugby. Kante ni mtoto wa kwanza na hivyo alitumia muda mwingi kupambana kusaidiana na wazazi wake waliokuwa ombaomba.

Kante

Kijiji cha Kante wengi wao walikuwa wasafisha mitaro na usafi wa jiji. Kiujumla waliishi uswahilini. Kante alizunguka jiji lao kwa zaidi ya kilometa 20 kwa siku kutafuta makopo na kwenda kuyauza ili kupata kipato

Kazi hiyo haikusaidia familia yao zaidi waliandamwa sana ukali wa maisha kutokana na ufukara wa kupindukia, Wakati wa kombe la dunia 1998 Kante alikuwa na miaka 7

Kante

Hakubahatika kuona mchezo wowote wa kombe la dunia aliishia kusikia majina makubwa ambao wengi walikuwa wahamiaji kutoka Afrika kama yeye.

Ilimpa faraja kuwa ipo siku anaweza kupitia njia hiyo. Waokota makopo wenzake walimuona chizi kwa kuwa na ndoto zile abadani Kombe la dunia ilikuwa fursa kubwa kwake kimaisha kwani alikuwa mfagiaji nje ya viwanja

Makopo yalipatikana kwa wingi sana biashara ilipamba moto alihakikisha anatembelea viwanja vingi kupata makopo ya kutosha baada ya Kombe la dunia shule ilimshinda kwa kukosa ada

Akiwa na miaka 8 akajiunga na klabu ndogo ya mtaani kwao ya JS Suresness. Wakamwona kioja kwenye timu kwani alidumaa sana halafu kafupi sana. Wachezaji walimcheka, wakidhani hakataweza kucheza dakika 90.

Kante

Mwanzoni alipewa dakika 10 za mwisho lakini akastaajabisha wengi Mwalimu wake anasema alifika kila sehemu ya uwanja. Alikuwa anacheza kama kichaa.

Kuna wakati kocha alimwambia asicheze sana akihofia asije akapata matatizo uwanjani. Hakushangilia walipotwaa kombe. Kutokana na umasikini klabu ikamwajiri awe anafundisha watoto ili aweze kusaidia familia yake kwa kibarua hicho

Baada ya baba yake kufariki, akijitokeza msamaria mwema Pierre Ville ambaye alimua kuchukua majukumu ya Kante Pierre akaanzisha safari ya Kante katika soka la kulipwa.


MAANA KAMILI YA USHINDI KATIKA KASINO ZA MERIDIANBETI NI PAMOJA NA MCHEZO WA PANDA PANDA.

Hii ndiyo burudani yenye ushindi! Ingia kwenye kasino ya Meridianbet kufukuzia ushindi huu. Cheza sasa Panda Panda na uwe moja ya washindi na Mabingwa.

Gomes, Gomes : Sitafanya Usajili wa Kutisha., Meridianbet

CHEZA HAPA

ONI MOJA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa