Kasa wa Njano Awapa Ubingwa wa CL Liverpool.

 

Kasa wa Njano, mwenye umri wa miaka thelathini, ambaye miaka kumi na mitano iliyopita alifika kwenye Uwanja wa Sea Life Aquarium huko Benalmádena (Málaga) kutoka Visiwa vya Cayman, ametabiri kuwa Liverpool itashinda fainali ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya Real Madrid Jumamosi mjini Paris.

 

Watunzaji wa kasa wa njano walitayarisha vyombo viwili tofauti vya umbali wa mita mbili huku kila kimoja kikiwa na jani la broccoli – ambalo liliwawakilisha wapinzani katika fainali hii – na, liliposhushwa ndani ya bwawa walikuwepo kasa, lilikwenda upande wake wa kushoto ambapo kulikuwa na picha ya timu ya Liverpool.

Kasa anatamani kuwa mwanafunzi bora wa wanyama wenye maono, kama vile pweza Paul, ambaye alijipatia umaarufu mwaka 2010 baada ya kutabiri kwa usahihi mechi nane za Kombe la Dunia 2010, ukiwemo ushindi wa Uhispania dhidi ya Uholanzi katika Fainali iliyochezwa Johannesburg, Afrika kusini mnamo Julai 11.

Mkurugenzi wa masoko wa Sea Life Benalmádena, María Morondo, alisema kuwa kasa wa Njano, ambaye ana uzani wa zaidi ya kilo 100, ni “the star of the Jurassic tunnel” na wageni wengi huumuulizia, ingawa anatumai kuwa katika hafla hii mnyama huyo amekosea ili timu ya Uhispania inayoongozwa na Carlo Ancelotti ishinde.


SHINDA SAMSUNG A32 NA AVIATOR

SHINDA Samsung A32 ukiwa na mchezo wa Aviator kwenye Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet! Kwea pipa ukusanye zawadi zako pamoja na ushindi mnono wa mkwanja!

 

SOMA ZAIDI HAPA

Acha ujumbe