Cedric Kaze, Kocha Mkuu wa Yanga amesema kuwa wachezaji wake wamekuwa wakifuata maelekezo ndani ya uwanja jambo linalowafanya wapate ushindi kwenye mechi zao huku akiweka wazi kuwa makosa waliyalofanya wapinzani wake yalikuwa faida kwao.

Jana, Desemba 6 Yanga ilisepa na pointi tatu muhimu Uwanja wa Mkapa kwa ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Ruvu Shooting na kuifanya ijikite kileleni ikiwa na pointi 31.

Kaze, Kaze Alivyoiua Ruvu Shooting, Meridianbet

Ikiwa imecheza jumla ya mechi 14 ndani ya Ligi Kuu Bara haijapoteza mchezo hata mmoja ndani ya dakika 90.

Kaze amesema:”Wachezaji wangu wanafuata maelekezo ndani ya uwanja jambo linalowafanya wanapata matokeo chanya hii ni furaha kwangu na kwao pia.

Kaze, Kaze Alivyoiua Ruvu Shooting, Meridianbet

“Kikubwa ambacho tunakitazama ni pointi tatu muhimu kisha baada ya kuzikusanya hizi tunatazama kipi tufanye ili kuwa bora zaidi kwa kuboresha makosa.

“Mashabiki pia wamekuwa wakitupa sapoti hii ni furaha pia inatufanya tuzidi kupambana ndani ya uwanja,” amesema.

Baada ya kushinda mchezo wake wa Kwanza kwa mwezi Desemba kigongo kinachofuata ni dhidi ya Mwadui FC.


MALIZA MWAKA KIBINGWA KWA KUJISHINDIA SHEA YAKO KWENYE SHILINGI 140,000,000TSH!!

Kipindi hiki cha sikukuu kinamalizika kwa namna ya kipekee. Shilingi 140,000,000 kushindaniwa katika michezo ya Evolution kwenye Kasino Mubashara ya Meridanbet. Ingia mchezoni na ujiwekee nafasi ya kushinda shea yako!!!

Kaze, Kaze Alivyoiua Ruvu Shooting, Meridianbet

SOMA ZAIDI

19 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa