Kazi Bado Sana Real Madrid -Zinedine Zidane

Meneja wa Real Madrid Zinedine Zidane anaona bado ana kazi kubwa sana ya kuifanya klabuni Real Madrid baada ya kichapo cha tatu bila dhidi ya PSG kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Zidane anasema alitarajia makubwa sana kutoka kwa kikosi chake wakati walipokijiandaa kupambana kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya. Hii imekuwa ni tofauti sana, huku baadhi ya mashabiki wa Real Madrid wakizomea kwa kumtaka aachie ngazi, hii ni kawaida kwa mashabiki wenye hasira timu inapofanya vibaya.

“Hatujakuwa kwenye kiwango tulichotarajia, lakini PSG wamecheza vizuri.” -Zidane

Zidane anaamini kuwa PSG waliwaadhibu, lakini hajapenda kukikosoa sana kikosi chake kwa kufanya vibaya dimbani.

Mabingwa wa Ligue 1, PSG waliwatawala vyema kwa dakika 90 na kufanya kama rekodi aliyoiweka meneja Zinedine Zidane kule Ulaya kuonekana si kitu kwa usiku wa mechi hiyo.

Zidane anasema kikosi kizima kinabeba jukumu na lawama za matokeo ya usiku huo na wanahitaji kufanyia kazi ili kujiboresha kwa mechi zijazo.

Makala iliyopita

Acha ujumbe