Kevin De Bruyne hajawahi kushinda tuzo ya mchezaji bora wa mwezi ndani ya ligi kuu ya Uingereza tangu atue kwenye ardhi hiyo ya mfalme Charles.

kevin bruyneKevin de Bruyne licha ya kucheza kwa kiwango kikubwa katika klabu ya Manchester City lakini mchezaji huyo hakuwahi kubeba tuzo ya mchezaji bora wa mwezi katika ligi hiyo jambo ambalo linawashangaza wengi imekuaje mchezaji huyo pamoja na ubora aliokua nao hajashinda tuzo hiyo.

Mchezaji huyo ameshinda tuzo ya mchezaji bora wa ligi hiyo kwa upande wa waandishi wa habari pamoja na shirikisho la soka nchini humo lakini bado kitendawili kwa Kevi de Bruyne imekua tuzo ya mchezaji bora wa mwezi wa ligi hiyo.

kevin de BruyneRaia huyo wa Ubelgiji ambae ameshacheza takribani misimu sita kwenye ligi hiyo na kupata mafanikio makubwa ikiwemo kushinda kila taji la ndani chini Uingereza yakiwemo mataji manne ya ligi kuu Uingereza na mataji mengine kama kombe la ligi pamoja na FA Cup.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa