Kibarua cha Scotland dhidi ya Belgium

Scotland anakutana na kibarua kizito wanapokutana na mmoja wa wapinzani wagumu katika soka lao la kimataifa Jumatatu wanapokutana uso kwa uso na Belgium kwenye hatua ya makundi kufuzu fainali za UEFA EURO 2020.

Gemu iliyopita Sctotland wameshindwa kabisa kuzuia kichapo dhidi ya Urusi na kujikuta wapo nafasi ya 4 kwenye kundi H. Bila shaka hii ni nafasi yao ya kurekebisha makosa ili waweze kupenya kufuzu michuano hii.

Belgium kwa upande wao ndiyo wanaounguruma kundini wakikamatia nafasi ya 1, wameshinda mechi zao zote na kuruhusu goli moja la kufungwa. Mechi yao ya mwisho walimuacha hoi San Marino Ijumaa kwa bao 4-0.

Kwa gemu walizokutana uso kwa Uso, Kombe la Dunia 2014, Belgium amekuwa kinara kwa kuongoza mechi zote nyumbani na ugenini kwa bao 2-0. Scotland hana bahati na wakali hawa.

John McGinn anaamini kuwa upande wake unakutana na kibarua kikubwa kwa mara nyingine na wanatarajia kufanya vyema kwa kuwa ni nafasi pekee ya kupata ushindi, pointi 3 ni muhimu mno kwao.

Acha ujumbe