Sasa daktari wa Diego Maradona, Leopoldo Luque anafanyiwa uchunguzi ikiwa anahusika na kifo cha legendari huyo wa soka.

Kuna wasi wasi kuwa huenda kulikuwa na aina ya uzembe ambao ulipelekea mauti ya Maradona.

Polisi wa mji wa Buenos Aires wamepatikana wakifanya upekuzi wa nyumba na kliniki ya daktari huyu kuona viashiria vyovyote vya uzembe juu ya matibabu aliyofanyiwa Maradona.
MWanasoka huyu aliyejijengea heshima kubwa aliripotiwa kufariki dunia kwa shinikizo la damu, wakati akiuguza jeraha baada ya kufanyiwa upasuaji.

Diego Maradona

Legendari huyu akiwa na umri wa miaka 60, akifanyiwa upasuaji kwenye mshipa ya ubongo akiwa na tatizo la kuganda kwa damu.

Upasuaji huu ulifanyika Novemba na kuripotiwa kuwa ilifanikiwa kikamilifu. Changamoto ya matumizi pombe ilifanya awe anapata matibabu pia.

Kwa mujibu wa BBC, polisi wanapofikia idadi ya 30 walitekeleza msako kwenye makazi ya daktari mapema Jumapili. Askari wengine wapatao 20 walivamia kliniki na kufanya uchunguzi.

Wakati zoezi hili likiagizwa na waendesha mashitaka ambao wana wasi wasi na siku za mwisho za maisha ya Maradona, bado daktari hajashitakiwa na yeye anakana kuhusika na kosa lolote zaidi ya kutekeleza majukumu yake ya kitabibu kwa uadilifu.


FURAHIA MUZIKI MTANDAONI HUKU UKITENGEZA MKWANJA!!

Mchezo wa Astro Legend unakupatia burudani ya muziki kupitia kasino ya mtandaoni ya Meridianbet. Utaburudika huku ukiendelea kutengeza mkwanja mrefu, jiunge sasa na uwe miongoni mwa mabingwa!!

Maradona, Kifo cha Maradona Chazua Gumzo Argentina, Meridianbet

INGIA MCHEZONI

15 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa