Kikosi bora cha ligi kuu ya Uingereza tayari kipo wazi huku ikishuhudia Manchester City wakinyanyua kombe la pili la ligi kuu hiyo. Kwa nafasi kubwa ameingiza idadi kubwa ya wachezaji ndani ya kikosi hicho ambacho kimesheheni majina makubwa na yaliyokuwa na nafasi kubwa ndani ya ligi hiyo.
Alisson Becker (Liverpool), safu hii ya kuidhibiti mipira yote inayopita katika lango anasimama raia wa Brazil ambaye ameleta uimara mkubwa ndani ya kikosi cha Majogoo msimu huu. Alitua kikosini mara baada ya Coutinho kuihama klabu hiyo na wakaamua kutumia pesa hizo kujaza nafasi zilizokuwa na mashimo makubwa kama hayo.
Trent Alexander-Arnold (Liverpool), upande wa kulia wa kikosi cha Majogoo umeimarika kwa kiasi kikubwa kutokana na uwepo wa nyota huyo mwenye umri mdogo na kasi ya ajabu ndani ya kikosi hicho. Msaada wake wa kutoa pasi za magoli 11 umewafikisha hapo wanapostahili.
Virgil van Dijk (Liverpool), ni mchezaji aliyeleta radha ya nini maana ya beki bora ndani ya kikosi chao. Kwa miaka mingi walikuwa na ugonjwa usiotibika katika eneo hilo lakini kwa sasa wameimarika. Uwezo wake wa kufunga, kutoa pasi na kuzuia vinamfanya kuwa beki bora zaidi ndani ya ligi hiyo.
Aymeric Laporte (Manchester City), raia huyo wa Ufaransa amekuwa muhimili wa kikosi cha Pep msimu huu. Hadi sasa ameruhusu magoli 22 pekee kupita hiyo ikiwa ni nafasi nyeti na kubwa sana kwa nyota huyo. Ana uwezo mkubwa wa kutoa pasi, kufunga na kuipanga safu yake vilivyo.
Andrew Robertson (Liverpool), kinda mwingine ndani ya kikosi hicho akifanya makubwa sana ambayo kwa nafasi moja au nyingine imechangia sana kuwaweka Liverpool nafasi ya juu. Pia, ana mchango mkubwa kama ule aliouonesha ndugu yake Anorld kwa kutoa pasi zipatazo 11 zote zikiwa ni za magoli.
Safu ya kiungo ikishikiliwa na watu wawili ambao ni: Fabinho (Liverpool) na Bernardo Silva (Manchester City) wawili hao wamekuwa kiunganishi kikubwa cha timu zao wakicheza soka safi eneo la katikati kuhakikisha timu pinzani hazioni kabisa mipira na kutoa pasi zinazoonekana na ambazo ni mwiba kwa wapinzani.
Eneo lililotisha zaidi ni lile la ushambuliaji likiwa na watu watatu ambao ni: Mohamed Salah (Liverpool), Raheem Sterling (Manchester City) na Eden Hazard (Chelsea). Nyota hawa wamekuwa chambo cha mafanikio ndani ya klabu zao wakifanya maajabu ya aina yake ndani ya vikosi vyao huku wakifunga idadi kubwa ya magoli na wengine kutoa msaada mkubwa wa wengine kufunga magoli.
Povel
Gud news