Mshambuliaji mpya wa Simba, Moses Phiri alishindwa kusafiri kwenda nchini Misri na timu hiyo kwajili ya maandalizi ya msimu ujao kutokana na kukosa Viza ya kusafiria ambayo imechelewa kupatikana.

Moses Phiri ni usajili mpya kwa Simba ambapo alikuwa wa kwanza kutambulishwa ndani ya timu hiyo akitokea katika klabu ya Zanaco ya nchini Zambia.

 

Moses Phiri

Kocha msaidizi wa Simba, Suleman Matola alisema kuwa kuna baadhi ya wachezaji wameshindwa kusafiri kwenda katika maandalizi ya msimu mpya kutokana na Visa kuchelewa kama Moses Phiri jambo ambalo litawafanya kusalia nchini lakini wachezaji hao watajiunga wakishapata visa zao.

“Kuna wachezaji bado hawajapata Visa kama Moses Phiri ambao kwa namna moja ama nyingine watabidi kusubiri kisha wakishapata waanze safari ya kuja Misri tayari kwaajili ya kuungana na wenzao nadhani haitachukuwa zaidi ya siku tatu watakuwa wameanza safari,”alisema kiongozi huyo.

Phiri alikuwa alikuwa anategemea kupara Viza yeke leo na haraka angeanza safari ya kwenda Misri.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa