Kipa wa Tottenham Hotspur FC, Antonin Kinsky, hatimaye amevunja ukimya wake baada ya usiku mgumu katika mechi ya UEFA Champions League ambapo Spurs walifungwa mabao 5-2 na Atletico Madrid. Kipa huyo mwenye umri wa miaka 22 alifanya makosa mawili ya mapema yaliyoigharimu timu yake mabao, hali iliyomfanya kocha wake kumtoa uwanjani baada ya dakika 17 pekee.

Makosa hayo yalianza dakika ya sita wakati Kinsky alipoteleza akiwa na mpira miguuni, na kumpa nafasi Marcos Llorente kufunga bao la kwanza kwa Atletico. Baadaye, alishindwa kuudhibiti mpira vizuri na kuruhusu Julian Alvarez kuongeza bao la tatu kwa wapinzani.

Baada ya mechi hiyo, Kinsky alitoa ujumbe kupitia Instagram akiwashukuru mashabiki waliomtumia maneno ya faraja. Katika ujumbe wake, alisema: “Asanteni kwa ujumbe wenu. Kutoka ndoto hadi jinamizi na kurudi ndoto tena. Tutaonana hivi karibuni.” Kauli hiyo ilionyesha azma yake ya kurejea kwa nguvu licha ya changamoto alizokutana nazo.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Kocha wa Spurs, Igor Tudor, alieleza kuwa alimtoa kipa huyo mapema ili kumlinda yeye na timu. Alisisitiza kuwa bado ana imani na uwezo wa Kinsky licha ya makosa yaliyotokea katika mechi hiyo muhimu.

Hata hivyo, uamuzi huo ulizua mjadala mkubwa, huku gwiji wa makipa Peter Schmeichel akimkosoa Tudor kwa kusema tukio hilo linaweza kuathiri kisaikolojia mustakabali wa kipa huyo kijana. Kinsky alijiunga na Spurs mwaka 2025 akitokea SK Slavia Prague kwa ada ya takribani euro milioni 16.5, lakini bado amekuwa akipata nafasi chache kutokana na uwepo wa kipa namba moja Guglielmo Vicario.


