Kisa Neymar Mashabiki Wamjia Juu Rais wa Palmeiras

Staa wa kimataifa wa Brazil Neymar ambaye kwasasa anakipiga katika klabu ya Al Hilal ya nchini Saudia Arabia amesababisha mashabiki wa soka nchini Brazil na duniani kote wamjie juu Rais wa klabu ya Palmeiras ya nchini Brazil anayefamika kama Leila.

Mashabiki hao wa soka wamechukiwa na kitendo cha Rais huyo kuongea maneno ambayo sio ya kiungwana kumhusu Neymar baada kuulizwa kama mchezaji huyo anaweza kujiunga nma klabu yake na ndipo Leila aliweza kutoa maneno ambayo sio ya kiungwana na kuwakera mashabiki wengi wa mpira nchini Brazil na duniani kwa ujumla.NeymarNeymar hatasajiliwa na Palmeiras, klabu hii si idara ya matibabu.”

“Nataka mchezaji atakayekuja na kujiunga mara moja, ambaye anaweza kucheza kesho ikiwa kocha atapenda.”

“Sitakubali tusajili mchezaji ambaye hayuko sawa kucheza.

Kauli hiyo imewakera mashabiki wa mpira kwani wameona kama Rais huyo amemkejeli staa huyo wa kimataifa wa Brazil kwa kile ambacho amekua akipitia, Wanaamini alipaswa kuongea kauli za kiungwana na kumtia moyo mchezaji huyo kutokana na majeraha yake badala ya kuanza kuongea kauli za kumvunja moyo na kumkejeli.

Acha ujumbe