Kizazi cha Dhahabu cha kilichoipa Heshima Manchester United

“Huwezi shinda chochote na watoto” , Yalikua ni maneno ya mchambuzi wa soka Allan Hansen baada ya Man Utd kufungwa goli 3-1 na Aston Villa mwaka 1995 , United walianza na vijana wadogo kama Phil Neville , Gary Neville , Nick Butt na Paul Scholes na baadae David Beckam na huu ndio ulikua mwanzo wa Fergie kuanza kuisumbua dunia na kizazi cha dhahabu . Vijana hawa walilelewa katika timu za watoto za United ivo walijua misingi na Falsafa za timu , walisumbua dunia hawa madogo na walimkosha sana Malikia hadi mwaka 1999 akampa jina la Sir babu . Mwaka 2002 madogo walimvuruga babu akaanza kuwauza na kutengeneza timu upyaa , kabla ya hawa walikuwepo Busby Babies walioleta utukufu Uingereza..

Baad ya kuvurugana na mmoja wa Maboss wa Liverpool Billy McConnel Sir Matty aliwaachia wahenga timu yao na kujiunga na wapinzani , alipofika Manchester Utd akatengeneza jeshi likaitwa Busby Babes na mwaka 1958 roho zao zikachukuliwa na ajali ya ndege . Kama ilivokua kizazi cha Ferguson Beckam na wenzake pia hiki kizazi kilikuzwa katika timu za watoto za Man Utd na walijua misingi na taratibu zote za timu ikiwemo kuichukia Liverpool , walikua ni vijana wenye vipaji vya kutisha waliokuja kuisumbua dunia ya mpira na walichukua ubingwa wa ligi mara mbili mfululizo 1956 na 1957 . Ndani ya Busby Babes walikuwepo kina Roger Bryne , Eddie Colman , Mark Jones , Duncan Edwards , Liam Whelan , Tommy Taylor , David Pegg na wengine wengi sanaa…

Wachezaji wa Man U waliopata ajali ya Ndege mwaka 1958

Kizazi kilitafutwa kukuzwa na kulelewa na Manchester United baadae wakaja kupewa madini na Matty Busby , walionekana watakuja kutisha zaidii ya mazimwi kwani dalili zilionyesha , kipindi wanachukua ubingwa mara mbili mfululizo walikua na wastani wa miaka 22 . Kizazi hichi cha balaa kilikuzwa chini ya skauti mkuu Joe Armstrong na msaidizi wake Jimmy Murphy walikusanywa kutoka maeneo mbalimbali na kukuzwa pamoja , jiji la Manchester ghafla waligubigwa na simanzi kubwa baada ya ndege iliyobeba vijana hao kuanguka wakitokea Yugoslavia kucheza mechi ya mzunguko wa pili robo fainali dhidi ya Red Star Belgrade na walifuzu nusu fainali….

Wakiwa katika ndege ya Airspeed Ambasador 2 iliyotengenezwa mwaka 1952 ilibidi wapiti Ujerumani kujaza mafuta , matatizo ya hali ya hewa anga kujaa na ukungu pia hitilafu mbalimbali za ndege zilisababishwa safari kuhairishwa , lakini jopo la wataalamu wa anga na mafundi wa ndege walijadili wa kina na kugundua kuna uwezekano wa safari kuanza baada ya kuchukua tahadhari kadhaa . Wasafiri wote waliokuwemo ndani ya ndege waliitwa tena baada ya kuanza kutawanyika , alisikika kiungo mshambuliaji Liam Whelan akisema “huenda hii ni siku yangu ya kufa lakini nipo tayari” .

Baada ya makubaliano yote na wasafiri wote kuingia ndani wakiwemo wachezaji , viongozi wa timu na benchi la ufundi na wengine wengi ndege ilishika barabara kukimbia kabla ya kupaa , kutokana na makubaliano yao walikubaliana waende Kilometre 2 kabla ya kupaa . Baada ya ndege kushika kasi zoezi la kuinyanyua likaanza kabla hawajafika mwisho wa barabara , jitihada za marubani kuirusha ndege zilionekana kugongwa mwamba huku ndege ikiwa katika kasi kubwa , alisikika rubani mmoja akisema “Yesu wangu tumeshindwa” , basi ndege iliuvaa ukuta uliozunguka uwanja wa ndege na kuondoka na makumi ya roho za watu….

Roho za kizazi cha dhahabu zilichukuliwa pale pale wachezaji nane walikufa eneo la ajali na mwingine alienda kufia hospitali , waliokufa ni Roger Bryne , Eddie Colman , Mark Jones , Duncan Edwards , Liam Whelan , Tommy Taylor , David Pegg , Geoff Bent . Johnny Berry na Jack Blancflower hawa kutokana na majeraha hawakuweza kucheza tena mpira , kocha Matty Busby alipata majeraha makubwa alilazwa na akapona , pia ajali ilichukua baadhi ya roho za viongozi wa timu.

Huu ndo ukawa mwisho wa kizazi cha Busby Babes vijana waliotabiliwa kutisha kama ukoma , wakati Busby babes wa kipotea kwa njia ya kifo hawa kina Beckam walipotea kwa njia ya kiburi . Busby alitegemea kutengeneza dunia yake kupitia hawa vijana lakini wenzao walianza kumvuruga mzee Fergie mpaka akaamua kuwauza mmoja mmoja . Baada ya ajali salamu za rambirambi zilitumwa sana lakini kubwa zaidi ilikua ya mahasimu wao Liverpool , walijitolea wachezaji watano muhimu wakachezee Man Utd huku wakiwalipa mshahara…

Baada ya kupona Matty Busby aliijenga upya United na kufanikiwa kuchukua European Cup mwaka 1968 , kama Ferguson alivoirudisha Man Utd kwenye ramani mwaka 2006 baada ya kuvurugana na kina Beckam

makala hii imeandaliwa na EZEKIA JOHN

17 Komentara

    Bonge la Historia, asante Meridianbet.

    Jibu

    👏👏

    Jibu

    meridianbet mpo juu kwa habar moto moto

    Jibu

    Meridian mko juu.

    Jibu

    Good news 👍

    Jibu

    meridianbet asante kwa taarifa nzuri

    Jibu

    Hao ni magwiji kweli wa sokawalioipatia sifa kubwa Manchester UTD safi sana #meridianbettz #meridianbet

    Jibu

    asante meridian kwa kutupa mambo mazuri

    Jibu

    man utd 1999 ilikuwa kizazi cha dhahabu vikombe vitatu ndani ya mwaka mmoja#meridianbet

    Jibu

    Hao ndo magwiji mpka leo nataman ijirudieh tena wamefanya poa sana kipind chao Asante meridian bet tz# meridian bet#

    Jibu

    Asanten meridianbet kwa kutupatia taarifa zilizo sahihi

    Jibu

    Fegie alikuwa mtu serious sana na falsafa zake “no player above the club”

    Jibu

    Hiyo ndo man u ambayo ulikua ukikutana nayo unatetemeka ila sio Sasa kweli mpira una badirika

    Jibu

    Kama kawaida yenu hamtuachi hata mara moja big up kwenu.

    Jibu

    Manchester walikuwa wako vizuri sana mpaka hasivi hakuna aliye ridhi vizazi vya nyuma

    Jibu

    Hii storia ipo pw sana

    Jibu

    Wametosha sana

    Jibu

Acha ujumbe