Katika mpira wa kisasa, idadi ya fulani ya mashabiki inapotokea kuifuatilia klabu fulani ni jambo ambalo kila shabiki hujisikia fahari zaidi ya kwenda kuangalia mechi uwanjani. Aina hii ya ushabiki imeshika kasi sana katika siku za usoni ikiwa na lengo la kuona thamani ya timu nje ya uwanja na namna watu wanavyopenda ripoti na taarifa mbalimbali kutoka kwenye timu husika. Klabu kubwa duniani pamoja na kuwa na mashabiki wengi zinafuatiliwa kwa kiwango kikubwa katika safu za mitandao ya kijamii; hii ikiwa ni Instagram, YouTube, Facebook, Twitter n.k.
Real Madrid wanaongoza wakiwa na idadi kubwa ya watu wanaofuatilia taarifa mbalimbali za klabu hiyo kwenye mitandao ya kijamii. Ana jumla ya wafuatiliaji 242.9M, ambapo amejipatia umaarufu huo mkubwa kutokana na historia yake kubwa ya kutwaa vikombe vyenye heshima kubwa. Akiwa na vikombe 13 vya klabu bingwa Ulaya na 33 vya ligi, kitu ambacho ni hatua nyeti na kama ataendelea hivyo ataendelea kukaa nafasi hiyo zaidi.
Barcelona wanafuatia wakiwa na jumla wafuatiliaji 240M. Wamejipatia umaarufu huo kutokana na kuwa na wachezaji maarufu na wenye majina makubwa duniani ambao waliweza kupita klabuni hapo kwa namna moja au nyingine. Baadhi ya majina makubwa yenye heshima kubwa hadi leo klabuni hapo ni Ronaldinho, Lionel Messi, Diego Maradona, Neymar, Xavi, Iniesta wote hawa wamesaidia kuijenga Barcelona hii inayofanya vizuri miaka ya hivi karibuni.
Uingereza nayo ipo katika ramani nzuri juu ya kufuatiliwa ambapo Manchester United wanashikilia nafasi ya tatu wakiwa na wafuatiliaji 137M; ambao idadi hiyo ni kubwa akiwa amemzidi Chelsea wafuatiliaji 47M ambaye kutoka Uingereza ndiye anayefuatia kwake. Hili ni halisi kabisa kutokana historia iliyojengwa na timu hiyo kwa miaka iliyopita katika ligi na klabu bingwa barani Ulaya.
Chelsea anashikilia nafasi ya nne akiwa na idadi ya 90.1M akipata umaarufu mkubwa kuanzia miaka ya 2003 baada ya kupata utawala mpya na mmiliki mpya Roman Abramovich ambaye alipigania kuifanya klabu hiyo kuwa bora na kutambulika zaidi ya ilivyokuwa mwanzo. Umaarufu wa klabu hiyo ulipanda kwa kasi baada ya kuanza kujizolea vikombe ambavyo hadi leo vinaipa heshima kubwa klabu hiyo na kuendelea kuonekana bora Uingereza.
Bayern Munich anafuata akiwa na jumla ya wafuatiliaji 79.2M. Idadi hiyo inaweza washangaza wengi kutokana na historia waliyonayo Wajerumani hawa, kwa sababu ni klabu inayofanya vizuri katika mitandao ya Facebook na Twitter, na kubwa zaidi kushangaa ni tofauti iliyopo kati yake na Arsenal ambayo ni ya wafuatiliaji 3M tu. Kama wataendelea kunyanyua vikombe watajiwekea nafasi nzuri zaidi ya kuongeza wafuatiliaji na mashabiki wengi duniani.
Klabu nyingine ni Arsenal yenye wafuatiliaji 76.2M, Manchester City yenye idadi ya wafuatiliaji 72.3M, Juventus wanashika nafasi ya nane wakiwa na 69.4M, Liverpool wanafuatia wakiwa na idadi ya 67.1M: na anayefunga nafasi ya kumi ni PSG akiwa na 66.7M.
Rehema
Asante kwa taarifa meridianbet