Saa chache tu baada ya Manchester City kutangazwa mabingwa wa EPL, kocha wa Liverpool aliibuka na kusema kuwa alimtumia ujumbe Pep na kumpongeza huku akimtafuta pia Gundogan ili kumpongeza kwa msimu mzuri aliokuwa nao.

Katika mazungumzo na waandishi wa habari kuelekea mechi yake dhidi ya Manchester United, Jurgen Klopp alieleza kuwa anaikubali sana Manchester City na kuwapongeza kwa ubingwa huku akimtaja Pep Guardiola kama kocha bora wa dunia.

Klopp awapongeza City
City wametangazwa mabingwa wa EPL kwa mara ya 5 ndani ya miaka 10

Klopp, ambaye ni kocha wa waliokuwa mabingwa watetezi wa EPL hakuonesha wivu wala hasira kufuatia kombe lake kuchukuliwa na City bali alifurahia na kuwapongeza na kukubali kuwa City wamekuwa vizuri sana msimu huu.

Ni mafanikio makubwa, hongereni, nilimtumia ujumbe Pep kumpongeza jana usiku na nilifanya hivyo kwa Ilkay. City imekuwa timu ngumu sana duniani. Walichokipata ni kikubwa na ukizingatia kwamba wamechukua mara 5 ndani ya miaka 10. Nahisi huwa inakuwa kwamba ukichanganya vyanzo vyako vya fedha na akili yako ya mpira basi unaweza kutengeneza kitu maalum na hichi ndo kilichotokea kwa City. City wanakikosi kizuri na kocha bora duniani, na hii itatengeneza timu bora sana,” alisema Jurgen.

Wadau wengi wanasema hawawezi kupingana na maoni ya Klopp kuhusu Pep kuwa kocha bora duniani ila ni mijadala ambayo inaweza kujadiliwa.

Manchester City watashuka dimbani mwishoni mwa mwezi huu kucheza na Chelsea ya Tuchel kwenye fainali ya ligi ya mabingwa ulaya kule Portugal. Vilevile, Liverpool watakuwa wanacheza na Manchester United leo ili kujaribu kukusanya alama waweze kuingia top 4.


PESA IPO HAPA KATIKA KASINO YA LUCKY LUCKY.

Hii ndiyo burudani yenye ushindi! Ingia kwenye kasino ya Meridianbet kufukuzia ushindi huu. Cheza sasa Lucky Lucky na uwe moja ya washindi na Mabingwa.

Klopp, Klopp Ampongeza Pep Na Gundogan Kwa Ubora!, Meridianbet

CHEZA HAPA

8 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa