Baada ya klabu ya Liverpool kutoa kipigo cha kikatili sana kwa klabu ya Bournemouth kwenye mchezo wa ligi kuu ya uingereza 9-0 siku ya Jumamosi, kocha wa klabu hiyo Klopp anaamini walikuwa na siku bora sana.

Michezo mitatu ya awali kwenye msimu 2022/23, klabu ya Liverpool wamefanikiwa kutoa sare mbili na kupoteza mchezo mmoja na kikosi cha Klopp kilijitahidi kucheza kadri ya uwezo wao ili waweze kurudisha hali ya ushindi kwenye mchezo wao dhidi ya Bournemouth.

Klopp, Klopp: Ulikuwa Mchana Bora sana Kwetu, Meridianbet

“Unapaswa kutoa njia ya nzuri ya uelekeao wa mchezo na ndivyo ninavyopenda sana kuanza leo, hatukusita, hatukuzuia, tulikwenda jumla jumla, tuliwapa presha, tulipambana katika eneo sahihi ndani ya box, nje ya box na pembeni box, mipila ya kipindi cha pili, tukaendela na aina hiyo.

“Mwishowe ulikuwa mchana mzuri wa soka kwetu, wafungaji wengi tofauti, yote haya, kisha, magoli yalikuwa mazuri, wakati mzuri na wote tunajua kuwa tulihitaji kitu kama hiki.” Alisema Klopp.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa