Klopp:Curtis Jones Kukipiga Dhidi ya Sheffield

Kocha wa klabu ya Liverpool Jurgen Klopp amesema kiungo wake raia wa kimataifa wa Uingereza Curtis Jones yuko tayari kwa mchezo wa kesho dhidi ya klabu ya Sheffield United.

Curtis Jones amekua nje kwa wiki kadhaa kutokana na majeraha ambayo yamekua yakimuandama kiungo huyo, Lakini kocha Klopp ameweka wazi mchezaji huyo yuko tayari kukipiga katika mchezo wa ligi kuu ya Uingereza dhidi ya Sheffield.kloppKurejea kwa kiungo Curtis Jones kunaenda kuimarisha safu ya kiungo ya klabu ya Liverpool na kuongeza machaguo zaidi, Hivi karibuni klabu hiyo ilikubwa na majeraha kwa wingi jambo ambalo liliiweka klabu hiyo kwenye wakati mgumu.

Kocha Jurgen Klopp pia ametoa taarifa za wachezaji wake wengine ambao walikua wanasumbuliwa na majeraha kama Diogo Jota na Trent Alexender Arnold, Huku akisema wachezaji hao wako katika sehemu ya timu lakini watakua tayari kua uwanjani wiki ijayo na sio katika mchezo wa kesho.kloppKocha huyo raia wa kimataifa wa Ujerumani hakuishia kueleza urejeo wa Curtis Jota, Trent, na Jota, Lakini pia aligusia jeraha la golikipa namba moja wa klabu hiyo Allison Becker na kusema anaendelea vizuri na anaweza kua sehemu ya timu wiki ijayo.

Acha ujumbe