Klose Kocha Msaidizi Bayern Munich

Mfungaji anayeongoza kwa wakati wote wa Ujerumani, Miroslav Klose ameteuliwa kuwa Kocha msaidizi wa Mabingwa wa Ujerumani, Bayern Munich kwa msimu ujao.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 41 amekuwa mkufunzi wa vijana kwenye Klabu hiyo kwa miaka miwili iliyopita baada ya kustaafu kama mchezaji mnamo 2016.

Alitumia misimu minne kama mchezaji wa Bayern kutoka 2007, akishinda ligi na vikombe vingine. Kocha mkuu wa Bayern, Hansi Flick, aliyetia saini kuwaongoza Miamba hao mwezi uliopita, alikuwa kocha msaidizi wa Ujerumani wakati Klose anaongoza mashambulizi kama Mchezaji kwenye Ubingwa wao wa Kombe la Dunia la 2014.

Klose alifunga mabao 71 katika michezo 137 kwa Ujerumani kati ya 2001 na 2014. Alicheza pia kwa Kaiserslautern, Werder Bremen na klabu ya Italia, Lazio.

Klose anajulikana sana kwa uchezaji wake bora na timu ya taifa ya Ujerumani. Alikuwa sehemu ya kikosi cha Ujerumani kilishinda Kombe la Dunia la 2014, hapo awali kilimaliza nafasi ya pili (2002) na ya tatu (2006, 2010) kwenye mashindano, na Kupoteza Fainali katika UEFA Euro 2008 na nafasi ya tatu katika UEFA Euro 2012.

28 Komentara

    Mchangako wako natumai utazaa matunda

    Jibu

    Mchango wake utazaa matunda

    Jibu

    Klose anajulikana sana kwa uchezaji wake bora. Yuko vzr sana.

    Jibu

    yuko vizur sana

    Jibu

    ni mwanzo mzuri kwake kuwa kocha

    Jibu

    Tunamkaribisha kocha mpya tunaitaji kazi nzuri

    Jibu

    Jamaa alikuwa vizuri sanaa

    Jibu

    Hongera kwake..

    Jibu

    karibu Bayern natumai hatoiangusha timu

    Jibu

    yuko vizuri sana taleta matunda

    Jibu

    Yuko vizur

    Jibu

    Yuko vizuri

    Jibu

    Jamaa alikua fundi Sanaa

    Jibu

    Namkubali sana

    Jibu

    ni jambo jema kwa close maana anaandaa mazingira ambayo yatamfanya awe bora kama walivyo wakima zizu

    Jibu

    Yupo vizur

    Jibu

    Yuko vizuri sana

    Jibu

    Mzee wa magoli ya vichwa. Asante meridian kutujuza mambo motomoto yanayoendelea ulimwenguni

    Jibu

    All the Best Klose on your new career.

    Jibu

    Ni Jambo la kheri kwa uongozi wa miamba ya soka la ujerumani kuheshimu na kumdhamini mchango wake aliotowak katika miamba hyo mm namtakiah mafanikio katika majukumu mapya ya kazi

    Jibu

    Atasaidia kuiinua zaidi bayern munich

    Jibu

    bonge la dili

    Jibu

    Yuko vizuri sana apige kazi tu

    Jibu

    Huyu jamaa analijua vizuri soka la ujerumani kuanzia ngazi ya vilabu mpaka timu ya taiga, kwahyo naona uwepo wake unaweza kuongeza kitu pale Bayern munich

    Jibu

    Ni mtu muhimu sana huyo Bayern munich

    Jibu

    Jamaa anafaa Sana kumsaidia

    Jibu

    Tunamkaribisha kocha mpya tunaitaji kazi nzuri

    Jibu

    Safi

    Jibu

Acha ujumbe