Justin Kluivert anasema kumuona mchezaji mwenzake na rafiki yake wa karibu Abdelhak Nouri akianguka uwanjani kwa Ajax mnamo 2017 ilikuwa wakati mbaya zaidi maishani mwake.
Mnamo mwaka wa 2017, Nouri, mwenye umri wa miaka 20 tu wakati huo, alipata shambulio la moyo katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Werder Bremen.
Nouri aliondoka hospitalini na kurudi nyumbani mwanzoni mwa 2020 lakini hakuweza kuendelea na kazi yake ya mpira wa miguu kutokana na uharibifu mkubwa katika Ubongo.
“Hiyo ilikuwa wakati mbaya zaidi maishani mwangu,” Kluivert anasema. “Nilishtuka tu, sikuamini.
“Sekunde moja bado unasimama naye uwanjani na unafanya mzaha na ya pili kila kitu ni tofauti. Ilitokea haraka sana.
“Nilitaka kuwa peke yangu [baadaye]. Mimi ni mtu ambaye huathirika na matukio kama haya. Niliwaza sana, niliendelea kujikumbusha nyakati nyingi nzuri tulizokuwa pamoja.
“Nimejifunza tena kwa njia mpya kwamba unapaswa kuthamini maisha kwa sababu yanaweza kubadilika kutoka wakati mmoja hadi mwingine.” aliongeza
Kluivert, ambaye kwasasa yupo kwa mkopo RB Leipzig, alikuwa mmoja wa wachezaji wa zamani wa Ajax, alivaa shati la zamani la Nouri 34 wakati alienda Roma mnamo 2018.
Treasure Heroes inakupa nafasi ya kupambania ushindi wako mkubwa kwenye kasino ya mtandaoni ya Meridianbet! Usisubiri hii, jiunge sasa kufurahia ushindi!
Pole yake
Pole sana
Polen sana
Poleni sana
Nice update
Pole sana
Pole sana
Ana wakati mgumu Sana wa majeraha
Pole sana
pole yake