Klabu ya KMC ya Dar es Salaam inayoshiriki ligi kuu ya NBC yainyima Simba alama tatu muhimu katika uwanja wa Benjamin Mkapa baada ya mchezo huo kumalizika kwa timu hizo kugawana alama moja moja huku kila timu ikifunga mabao mawili  mawili.

Imekuwa ni mara ya kwanza kwa Kmc kupata alama moja kwa Simba katika mechi ambazo wamewahi kukutana. Katika mechi 8 ambazo walicheza Kmc alipoteza mechi zote bila hata kupata sare na sasa ndipo katika mechi yake ya tisa amepata alama moja  akiwa ugenini.

Kmc ilitokea nyuma baada ya kufungwa bao la mapema kabisa na Simba ambalo lilitupiwa kimyani na Moses Phiri ambaye amekuwa na muda mzuri toka ajiunge na wekundu hao kwani mechi zote alizocheza ametupia kambani.

KMC, KMC Atamba zaidi Dhidi ya Simba, Awakosesha Alama 3!, Meridianbet

Baada ya kurudi katika mapumziko Wanakino Boys waliingia na moto uwanjani na kusawazisha bao kupitia kwa Matteo Antony dakika ya 47, wakati Simba bado wakishangaa ndani ya dakika 10, George Makang’a anapachika bao la uongozi kwa upande wa Kmc na baadae Simba kusawazisha bao la pili katika dakika za jioni kupitia kwa Habib Kyombo na kufanya mchezo kumalizika kwa  sare ya 2-2.

KMC ambayo ipo chini ya kocha wake mkuu Thierry Hitimana imekuwa haina mwendelezo mzuri wa matokeo ndani ya NBC kwani  katika mechi tatu alizocheza amepata sare mbili na amepoteza mchezo mmoja, hajashinda mchezo wowote  huku akiwa katika nafasi ya 11 ya msimamo.

Hitamana amewahi kufundisha vilabu mbalimbali hapa Tanzania ikiwemo Namungo, Mtibwa na nyinginezo. Mechi ijayo atamenyana na Ihefu ambayo itakuwa ni tarehe 17 mwezi huu.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa