Klabu ya Kmc leo hii itamkaribisha Ihefu kwaajili ya kucheza mchezo wao wa ligi kuu ya NBC ambao ni mchezo wa mzunguko wa nne huku timu nyingine nyingi zikiwa tayari zimeshacheza mchezo huo wa raundi ya nne.

 

Kmc Kumkaribisha Ihefu

 

Kmc ambayo inaongozwa na Thierry Hitimana bado mpaka sasa hawajashinda mchezo wowote katika mechi zao tatu walizocheza, leo wataingia uwanjani kujiuliza kwa Ihefu ambao ndiye anashikilia mkia kwenye msimamo mpaka sasa akiwa kapoteza mechi zote tatu.

Ihefu ambao wamepanda daraja msimu huu baada ya kushuka msimu uliopita wameanza vibaya msimu huu ukilinganisha na msimu juzi ambapo walianza kwa kuleta ushindani kwenye ligi kuu imekuwa tofauti na walivyoanza.

 

Kmc Kumkaribisha Ihefu

Kmc mpaka sasa kwenye hiyo michezo mitatu hajashindaa mchezo wowote, kapata sare mbili na amepoteza mchezo mmoja, wakati Ihefu akiwa hana alama yoyote mpaka sasa. Na michezo ya mwisho kukutana ya Ligi kuu ya Tanzania Bara kila mmoja alichukua alama tatu akiwa nyumbani kwake na leo zinakutana timu ambazo hazijashinda mchezo wowote majira ya saa 10 jioni.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa