KMC Yavunja Ukame Wa Ushindi Kwa Kuwachapa 1-0 Mashujaa

Hatimaye tabasamu limerejea kwa KMC FC baada ya kipindi kirefu cha kusota bila ushindi. Timu hiyo imeonja ladha ya pointi tatu kwa mara ya pili msimu huu kufuatia ushindi mwembamba wa bao 1-0 dhidi ya Mashujaa. Ni ushindi wa pili msimu huu kwa KMC ambao wamekua wakiandamwa na matokeo mabovu.

Mchezo huo ulipigwa Uwanja wa Majaliwa, Ruangwa mkoani Lindi, ambao KMC wameuchagua kwa muda kama uwanja wao wa nyumbani baada ya KMC Complex kufungwa kupisha matengenezo. Ndani ya mazingira mapya, KMC walionekana na kiu ya ushindi na wakaupata.

KMC Yavunja Ukame Wa Ushindi Kwa Kuwachapa 1-0 Mashujaa

Shujaa wa siku alikuwa ni mshambuliaji Daruweshi Saliboko aliyepachika bao pekee dakika ya 22, bao lililotosha kuwapa pointi tatu muhimu. Kwa ushindi huo, KMC sasa wanafikisha pointi nane baada ya mechi 13, japo bado wanabaki mkiani mwa msimamo, lakini matumaini ya kuamka upya yameanza.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

Kwa upande wa Mashujaa, kichapo hicho kinawaacha wakiwa na pointi 13 baada ya mechi 12, wakishika nafasi ya 10 kwenye msimamo wa ligi. Ni pigo dogo, lakini bado wapo kwenye nafasi ya kujipanga upya.

KMC Yavunja Ukame Wa Ushindi Kwa Kuwachapa 1-0 Mashujaa

Katika mchezo mwingine uliochezwa jana mchana Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya, Mbeya City na Dodoma Jiji FC walitoshana nguvu kwa sare ya 1-1. William Edgar aliitanguliza Dodoma Jiji dakika ya 10 kabla ya Eliud Ambokile kuisawazishia Mbeya City dakika ya 26. Matokeo hayo yameifanya Mbeya City kufikisha pointi 10 na kupanda hadi nafasi ya 13, huku Dodoma Jiji wakifikisha pointi 14 na kupanda hadi nafasi ya nane. Ligi inaendelea kupamba moto.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.