Timu ya KMKM ya Zanzibar imefanikiwa kunyakua ubingwa wa ligi kuu ya Zanzibar ikiwa na alama 44 katika michezo 22 iliyocheza.

Mabingwa hao wa Zanzibar wamechukua kombe hilo la Ligi kwa mara ya 7 sasa. KMKM walipewa jana kombe hilo la ligi kwa msimu wa 2020.2021. Ushindi huo ulikuja baada ya kufunga timu ya Black Sailors 2-0.

KMKM itawakilisha Zanzibar katika kombe la klabu bingwa barani Afrika msimu wa 2021/2022. Jioni ya jana ndio ilikuwa siku ya mwisho wa michuano hiyo yenye mechi 22 tu, huku ikiwa na wawekezaji au wadhamini wachache mno!

KMKM
Nahodha wa KMKM akipokea kombe

Msimamo umemalizika hivi, Bingwa (KMKM) Wamepewa Kombe na Medali ambapo Wataiwakilisha Zanzibar katika mashindano ya Klabu Bingwa Barani Afrika msimu wa mwaka 2021-2022.

Timu 2 za chini zimeshuka Daraja Hard Rock kwenda kucheza Ligi Daraja la Kwanza Kanda ya Pemba na Chuoni kushuka Daraja la kwanza Kanda ya Unguja.

Wadau wengi wa soka Zanzibar wameshukuru kumaliza ligi, ila wanatamani sana kupata wadhamini zaidi kwa kuwa kumekuwa na changamoto ya kukosa Udhamini ambapo kumesababisha kukosekana hamasa ya Ligi.


WEKA PESA KUPITIA DUKANI MERIDIANBET!

Chukua namba yako ya akaunti na kiasi cha pesa unachotaka kuweka, sogea kwenye duka lolote la Meridianbet lililo karibu nawe utasaidiwa kuweka pesa.

Weka Pesa Meridianbet

WEKA PESA

4 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa