Kobbie Mainoo Aendelea Kutamba Euro 2024

Kiungo kinda mwenye umri wa miaka (19) Kobbie Mainoo ambaye yupo na kikosi cha timu ya taifa ya Uingereza kwenye michuano ya Euro ameendelea kufanya vizuri kwenye michuano hiyo.

Kiungo Kobbie Mainoo amefanikiwa kuanza kwenye michezo miwili ya ligi kuu ya Uingereza ambayo imekua muhimu kwa taifa hilo, Kwani michezo ilikua ya hatua ya 16 bora na robo fainali kiungo huyo alifanikiwa kucheza kwa kiwango kikubwa katika michezo hiyo.kobbie mainooKijana huyo mzaliwa wa jiji la Manchester amefanikiwa kutengeneza rekodi ambayo haijawahi kutokea tangu mwaka 1980 kwenye michuano ya ulaya, Kwani amefanikiwa na wastani wa kupiga pasi sahihi kwa asilimia 96% akipiga pasi sahihi 133 kati ya pasi 138 alizopiga kwenye michuano hiyo kuliko mchezaji mwingine yeyote.

Kutokana na ubora ambao ameuonesha Kobbie Mainoo kwenye michezo miwili ya mwisho kwenye kikosi cha Uingereza ni wazi ataanza kwenye mchezo wa nusu fainali hapo kesho dhidi ya timu ya taifa ya Uholanzi, Licha ya umri wake kua mdogo lakini kiungo huyo anaendelea kuwashangaza watu kila siku kutokana na kiwango cha cha juu anachoonesha.

Acha ujumbe