Kocha Mkuu wa Al Hilal Omdurman kutoka Sudan, Florent Ibenge, anaripotiwa kufikia makubaliano na klabu ya Azam FC na sasa anatazamiwa kujiunga rasmi na benchi la ufundi kwa msimu wa 2025/26.
Taarifa zinaeleza kuwa mkataba huo umefikiwa kwa ajili ya msimu unaokuja, ambao unatarajiwa kuwa na ushindani mkali ndani ya Ligi Kuu Tanzania Bara. Azam FC, ambao walimaliza msimu wa 2024/25 katika nafasi ya tatu kwa pointi 63, wameamua kuimarisha kikosi chao baada ya kumaliza msimu bila taji lolote licha ya kufunga mabao 56.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Kuna dalili kuwa Kocha huyo atatua nchini hivi karibuni kwa ajili ya kuanza majukumu yake rasmi, huku Azam FC wakiendelea kutumia dimba la Azam Complex kama uwanja wao wa nyumbani.
Akizungumzia taarifa hizo, Mkuu wa Idara ya Habari wa Azam FC, Zakaria Thabit maarufu kama Zakazakazi, amesema:
“Hata mimi ninaskia kuhusu taarifa hizo ambazo unauliza. Kwa hiyo kama kutakuwa na taarifa yoyote kwenye upande wetu, basi jambo hilo litakuwa wazi na litafahamika, hakuna kitakachofichwa.”
Mashabiki wa Azam FC sasa wanasubiri kwa hamu kuthibitishwa kwa ujio wa kocha huyo aliyewahi kufanya vizuri na timu za AS Vita na timu ya taifa ya DR Congo, wakitarajia atawapa mafanikio ya kweli msimu ujao.