Kocha wa timu ya taifa ya Ujerumani Hans Flick ameita kikosi cha timu ya taifa ya Ujerumani ambacho kitashiriki michezo kadhaa ya kirafiki ambayo timu hiyo itacheza huku akiwaacha mastaa kadhaa kwenye timu hiyo.
Kocha Flick amewapa nafasi vijana watano wapya kwenye timu ya taifa ambao watakua wakiitumikia timu hiyo kwa mara ya kwanza katika michezo miwili ijayo ambayo itakua kati ya Peru na Ubelgiji, Wachezaji kama Rudiger na Leroy Sane watakosekana katika mchezo huo.Wachezaji wapya ambao wataitumikia timu ya taifa ya Ujerumani kwa mara ya kwanza ni Josha Vagnoman, Marius Wolf, Mergim Berisha, Kevin Schade, naFelix Nmecha Flick anaangazia kuwapa vijana wapya nafasi zaidi katika michezo hiyo ya Ujerumani.
Wachezaji 15 tu ndio waliofanikiwa kuitwa tena kwenye kikosi cha kocha Flick kati ya wachezaji 26 walioitwa kwenye michuano ya kombe la dunia mwaka 2022, Ni wazi timu hiyo inapanga kutengeneza kikosi kipya chenye vijana wengi ambao watakua na msaada wa taifa hilo siku za mbeleni.Kocha Flick anasema lengo kuu ni kujiandaa na kuwaweka pamoja wachezaji mapema kwajili ya michuano ya mataifa ya Ulaya mwaka 2024, Huku akisisitiza ni jambo zuri kutengeneza timu imara kupitia michezo ya awali ya kimataifa kwajili ya kuingiza wachezaji wapya kwenye kikosi.