Kocha wa Uholanzi, Ronald Koeman Amelazwa!

Imeripotiwa kutokea huko THE HAGUE, Netherlands kuwa kocha mkuu wa kikosi cha timu ya taifa Dutch, Ronald Koeman alihitaji matibabu zaidi na kukimbizwa hospitalini kutokana na tatizo la mshtuko wa moyo.

Mke wake alizungumza juu ya hali ya kiafya ya kocha huyo kwa gazeti la De Telegraaf siku ya Jumapili mwishoni mwa wiki iliyopita.

Kocha huyo mwenye umri wa miaka 57 kwa sasa alipatwa na tatizo la ugonjwa wa moyo ambapo akatakiwa kukimbizwa hospitalini huko Amsterdam ikiwa ni mara baada ya kutopata nafuu wakati akiwa nyumbani kwake.

“Alivyowahishwa hospitalini na kwa kuhudumiwa vyema na madaktari tuliowakuta ilisaidia sana hali yake kuendelea kuwa sawa kabisa,” alisema hayo Bartina Koeman.

Koeman, amekuwa na kikosi cha taifa cha Dutch tangu mwaka 2018, na akategemewa kuruhusiwa kwenda nyumbani kutoka hospitalini siku ya leo.

“Ilikuwa ni mshtuko!” Shirikisho la Kandanda la taifa la Uholanzi liliandika hivi kupitia mtandao wao wa Twitter.

“Tunayo furaha, mambo yamekuwa vyema zaidi. Nguvu anazo na kocha huyo anaendelea kupata nafuu zaidi.”

Imeripotiwa kutokea huko THE HAGUE, Netherlands kuwa kocha mkuu wa kikosi cha timu ya taifa Dutch, Ronald Koeman alihitaji matibabu zaidi na kukimbizwa hospitalini kutokana na tatizo la mshtuko wa moyo.

Enzi za ujana wake Koeman, alikuwa akikipiga kwa klabu za Ajax, PSV, Feyenoord na klabu ya soka ya Barcelona pamoja na timu ya taifa kote huko akiwa kama mlinzi. Kwa sasa ameshakiwezesha kikosi chake kufuzu kuingia kwenye michuano ya Euro 2020 akiwa na taifa lake la Uholanzi.

Hata hivyo, michuano imeahirishwa kwa sasa na kusogezwa hadi mwaka 2021 itakapofanyika kama ilivyopangwa mwanzo.

21 Komentara

    Utapona mzee.

    Jibu

    Atapona tu Mungu ni mkubwa

    Jibu

    Mungu atakusaidia utakuwa poa

    Jibu

    Utakuwa salama

    Jibu

    Atapona tu pole yake

    Jibu

    Inshallah utapona

    Jibu

    Mungu ata mjalia atapona

    Jibu

    Mungu hatamsaidia hatapona

    Jibu

    Atapona mungu amsaidie tu

    Jibu

    mwenyezi mungu ndo muweza wa kila kitu atapona na atarudi ktk hal yk ya kawaida

    Jibu

    Mungu atamsaidia atapona

    Jibu

    atapona2

    Jibu

    Atapona tu

    Jibu

    tunamuombea kwa Mungu apone aendelee na majukumu yake ya kimichezo

    Jibu

    Mwenyezi mungu atamuafu.

    Jibu

    Utampona 🙏

    Jibu

    Mungu amsaidie apone haraka aendelee na majukumu yake

    Jibu

    Pole sana Dutch

    Jibu

    Mungu amponye aendelee na majukumu yake..

    Jibu

    Mungu amjalie aendelee na majukumu yake

    Jibu

    Hakika utapona.na utarudi kwenye hari yako kama zamaniii

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.