KOCHA YANGA APATA UBARIDI KISA NAMUNGO

KUELEKEA kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Namungo unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Majaliwa, Kocha Mkuu wa Yanga ameweka wazi kuwa wanakabiliwa na mchezo mgumu watapambana kupata pointi tatu muhimu.

Saed Ramovi amebainisha kuwa maandalizi yapo vizuri na wapo tayari kwa ajili ya mchezo huo ambao utakuwa na ushindani mkubwa na malengo ni kuona wanapata pointi tatu muhimu.KOCHA

“Tuna mchezo mgumu mbele yetu, katika maandalizi yetu mpaka sasa kila kitu kipo vizuri, tunafahamu Namungo wana wachezaji wazoefu lakini sisi hatupo hapa kutafuta kingine zaidi ya alama tatu.

“Ni jambo la kujivunia kuwa hapa, nawashukuru mashabiki wa Yanga wanaotoka Dar. Mashabiki wamekuwa na moyo kwa kuwa wapo pamoja na timu kila mahali hivyo nasi tunapaswa kuwapa furaha kwa kupata ushindi.”

Kwa upande wa nyota wa Yanga, Dennis Nkane amesema kuwa wachezaji wanatambua umuhimu wa mchezo huo na wapo tayari kupata pointi tatu.

“Sisi wachezaji tunatambua umuhimu wa alama tatu kwenye ligi, tumekaa chini na kuzungumza wapi kwa kuboresha, tunamsikiliza mwalimu na kujituma kwa dhati ili kuhakikisha tunapata matokeo mazuri, mchezo wa kesho ni mgumu lakini tupo kwaajili ya kupambana na kushinda.”

Acha ujumbe