Kocha wa Barcelona Ronald Koeman amenukuliwa akipingana na raisi wa mpito wa klabu hiyo – Carlos Tusquets baada ya kusema angemuuza Messi majira ya kiangazi.

Siku ya Ijumaa, Tusquets alinukuliwa akitoa maneno hayo ambayo alidai kwa sababu za kiuchumi, majira ya kiangazi yalikuwa sahihi zaidi kumuuza Messi. Kwa Tusquets, ingepunguza fedha nyingi za mshahara pamoja na kuongezea timu mapato.

Kwa Koeman, hii sio sahihi. Akizungumza na waandishi wa habari, kocha huyo amesema ” tunafahamu hali ya Messi. Kama kuna mtu yeyote ambaye anapaswa kuamua hatma yake, basi ni yeye [Lionel Messi] mwenyewe.

“Sijali kinachosemwa nje ya klabu, lakini maneno yanayosemwa ndani ya klabu hayatusaidii kuwa watulivu na kufanya kazi yetu. Hatuwezi kuzuia ya nje ila ya ndani hiyo ni habari nyingine.

“Kama kumuuza Messi majira ya kiangazi ni maoni binafsi ya Tusquets, ninaheshimu hilo, lakini Leo mwaka mmoja kwenye mkataba wake na yeye ndiye atakayefanya maamuzi.”


FURAHIA MUZIKI MTANDAONI HUKU UKITENGEZA MKWANJA!!

Mchezo wa Astro Legend unakupatia burudani ya muziki kupitia kasino ya mtandaoni ya Meridianbet. Utaburudika huku ukiendelea kutengeza mkwanja mrefu, jiunge sasa na uwe miongoni mwa mabingwa!!

Koeman, Koeman Azungumzia Suala la Messi., Meridianbet

INGIA MCHEZONI

20 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa