Koeman: Natamani Kumuona Messi Akicheza na Neymar

KOCHA wa Barcelona, Ronald Koeman, anaamini kuwa Barcelona itafanya kitu kuona msimu ujao Lionel Messi anacheza tena na Neymar ndani ya Camp Nou.

Hii ni baada ya hivi karibuni, Neymar kutamka wazi kuwa msimu ujao anataka kucheza tena na Messi ingawa haijaelezwa wapi kama ni PSG au Barcelona.

Neymar aliondoka Barcelona mwaka 2017 na kutua PSG. Alicheza na Messi ndani ya Barcelona kuanzia 2013, tangu msimu uliopita, staa huyo amekuwa akihusishwa kurejea viunga vya Camp Nou.

Nyota Messi mkataba wake unatarajiwa kumalizika mwishoni mwa msimu huu ambapo awali naye alikuwa anahitaji kusepa ndani ya kikosi hicho.

“Kila mmoja anafahamu suala la Messi, mtu pekee ambaye anayeweza kuamua hatma yake kwa sasa ni yeye mwenyewe.

“Klabu inapambana kuona inakuwa na wachezaji bora , nataka kuona Messi anacheza hapa na mchezaji bora (Neymar) ndani ya Camp Nou itakuwa vizuri zaidi,” amesema Koeman.


MALIZA MWAKA KIBINGWA KWA KUJISHINDIA SHEA YAKO KWENYE SHILINGI 140,000,000TSH!!

Kipindi hiki cha sikukuu kinamalizika kwa namna ya kipekee. Shilingi 140,000,000 kushindaniwa katika michezo ya Evolution kwenye Kasino Mubashara ya Meridanbet. Ingia mchezoni na ujiwekee nafasi ya kushinda shea yako!!!

SOMA ZAIDI

14 Komentara

    Wakifanya ivyo itakuwa poa sana miamba wawili wakikutana

    Jibu

    Itakuwa poa sna Messi na Neymar watamani kucheza wote kwa Mara nyingine

    Jibu

    Bila shaka Koeman alielewa kwamba alichomaanisha Neymar anajaribu kuweka mambo sawa upande wao

    Jibu

    Nafikiri yuko sasa kwake kusema hiyo ila kwa upande wa wachezaji hao sidhani kama itakuwa hivyo kutokana na changamoto walizopitia ingawa kwa sisi mashabiki tutafirahi zaidi kama watakuwa pamoja

    Jibu

    itakua vizuri

    Jibu

    Itapendeza kwakwel

    Jibu

    Itakuwa vyema sana

    Jibu

    Itakua poa sana hiyo wakikutana Timu moja

    Jibu

    Kombineshen makin itarud tena

    Jibu

    Gud idea

    Jibu

    Itakuwa poa Sana

    Jibu

    Safi

    Jibu

    Itakua poa mnooo

    Jibu

    Huyu Koeman nae baada alete ushindi anaanza kumtaman neymar

    Jibu

Acha ujumbe