Kombe la dunia ambalo hufanyika kwa kipindi maalum kutoka kwenye muda ambao unajulikana duniani kote mara nyingi huibua burudani ya aina yake kutokana na timu nyingi kujupanga kimashindano ili kuweza kujaribu kupeleka heshima kwenye mataifa yao. Jambo ambalo hufurahisha zaidi ni maandalizi kuelekea michezo hiyo ya fainali.
Huku hadi sasa hatua ya kusaka tiketi ikiwa inaendelea kwa mataifa mbalimbali yatakayotaka kuonesha ushiriki ndani ya ligi hiyo; wenyeji wetu ambao ndio waandaaji wa mashindano bado wanajiweka vizuri ili kuhakikisha kwamba kila taifa ambalo litashiriki nchini humo linapata mapokezi makubwa na ya aina yake.
Jambo kubwa zaidi ni taifa hilo la Qatar ambalo ndio mwenyeji wa masuindano hayo kuzindua vitu mbalimbali vinavyoendana na kasi nzima ya mashindano hayo makubwa ikiwemo ufunguzi wa viwanja na hata maandalizi ya miundombinu rafiki kwa ajili ya timu shiriki kuweza kupata mazingira rafiki ya ukaaji wao nchini humo.
Siku za hivi karibuni waandaaji wa kombe hilo kwa msimu huu wakishirikiana na shirikisho la soka duniani waliweza kuzindua nembo ambayo ni ya aina yake na itakayotumika kwenye mashindano ya msimu huu kama kielelezo cha kuweza kuweka mambo yaanze kutangazwa mapema hadi pale itakapofika 2022.
Nembo hiyo imewekwa kuwa ya kipekee sana na ikiwa na maana kubwa sana kwa taifa la Qatar ikiwa na umbo namba nane [8] ambalo linaakisi tafsiri ya pekee yenye kuupa hadhi uwanja ambao umejengwa kisasa nchini humo wenye umbo namba nane. Na ambao unakadiriwa kuwa na uwezo mkubwa sana wa kubeba watu.
Ndani ya nembo hiyo kuna maua yamewekwa ambayo ni kiakisi kikubwa cha utamaduni halisi wa taifa hilo yaani ikiweza kuusifia na kuuenzi utamaduni wao. Pia kuna alama ya mpira ndani yake. Mbali na hilo kuna alama nyingine ya alama za kiarabu ikiwa bado ni sehemu inayoakisi heshima ya taifa hilo na mataifa mengine ya Uarabuni.
Mashabiki wengine wameonekana kuridhishwa sana na aina ya nembo ambayo imeweza kubuniwa kwa ajili ya mashindano hayo. Kwa sababu ni ubunifu wa hali ya juu ambao haujaweza kuhusisha kabisa suala zima la kunakili nembo nyingine za mashindano yaliyokwisha kupita.
Furahav
Tunalingojea vizuri.