Barcelona wamepanga kumuacha kiungo ambaye ni mmoja wa viungo wanaowathamii sana Konrad de la Fuente aondoke kwa mkopo msimu ujao.

Ronald Koeman alimpa nafasi ya kucheza kwenye kikosi cha kwanza cha kwanza msimu uliopita akishiriki kwenye Copa del Rey na Ligi ya Mabingwa mnamo 2020/21.

Licha ya kutajwa kama nmchezaji muhimu kwa siku zijazo za kilabu, Koeman bado haoni kama staa huyu anahitajika kwenye kikosi chake cha kwanza na anataka kumpa nafasi katika kiwango cha juu.

Konrad de la Fuente Kuondoka Barca kwa Mkopo!

Kwa mujibu wa ripoti kutoka Marca, Kocha huyo Mholanzi sasa ameamua kuwa de la Fuente angefaidika zaidi ikiwa ataondoka kwa mkopo kwa miezi 12 ijayo kuliko kubaki Catalonia.

Ripoti hiyo inasema Koeman tayari amekutana na wawakilishi wa nyota huyo wa miaka 19 kujadili hatua hiyo na ofa zilizo mezani kutoka England, Ujerumani na Ufaransa.

Licha ya uwezekano wa kutoka kwa mkopo, Koeman haoni uwezekano wa kuidhinisha kifungu cha ununuzi katika makubaliano yoyote, na de la Fuente akiwa ni sehemu ya mpango wake wa muda mrefu huko Camp Nou.


WEKA PESA KUPITIA DUKANI MERIDIANBET!

Chukua namba yako ya akaunti na kiasi cha pesa unachotaka kuweka, sogea kwenye duka lolote la Meridianbet lililo karibu nawe utasaidiwa kuweka pesa.

Weka Pesa Meridianbet

WEKA PESA

ONI MOJA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa