Korir na Rotich Waibeba Kenya Olimpiki.

 

Mkimbiaji, Emmanuel Korir ameishindia Kenya medali ya kwanza ya dhahabu katika mashindano yanayoendelea ya Olimpiki huko Japan baada ya kushinda mbio za mita 800 na kumuongoza mkenya mwingine Ferguson Rotich kumaliza wa pili na kushinda nishani ya fedha.

 

Korir alimaliza mbio hizo kwa muda wa 1:45.06 kuhakikisha Kenya inasalia na taji hilo kwenye mbio hizo za mizunguko miwili ambazo David Rudisha alishinda miaka mitano iliyopita. Rotich alimaliza kwa muda 1:45.23 ili kushinda medali ya fedha .

Kwingineko katika mbio za mita 3000 kuruka viunzi kwa upande wa akina dada mkenya Hyvin Kiyeng alimaliza wa tatu na kujishindia medali ya shaba .

Mkenya huyo alimaliza kwa muda wa 9:05.39 katika mbio ambazo Mganda Peruth Chemutai alishinda dhahabu alipotimka mita 300 za mwisho kumpita Mmarekani Courtney Frerichs ambaye alikuwa ameongoza katika raundi mbili lakini akalazimika kujishindia medali ya fedha.


VUNA MKWANJA NA KASINO ZA MERIDIANBET!

Unakila sababu ya kuwa moja ya mamilionea katika kasino za mtandaoni za meridianbettz, Mchezo wa Ruby Casino Queen unaweza kukufanya ujishindie mkwanja mrefu. Furahia ubora wa kasino zetu na njia kibao za kuwa mshindi leo hii ukiwa na mrembo Ruby.!

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA SASA

Acha ujumbe