Koulibaly: Bado Naipenda Napoli

Kuna wakati huwa inakuwa ni vigumu kuwaamini wachezaji wakiwa wanaongea wazi tu juu ya mapenzi yao katika klabu wanazozicheza kwa sababu maisha ya kisoka yamegubikwa na masuala ya kifedha sana tofauti na vile watu wanavyodhani kwamba mchezaji anaweza kusalia katika klabu fulani endapo ataoneshwa maslahi zaidi nje ya pale.

Wachezaji wengi sana huwa na usemi huu wa juu ya kusalia katika vilabu vyao kwa kipindi kirefu zaidi lakini hupata ushawishi wa kimaslahi na hata kimafanikio kwa sababu ubora wa mchezaji huongezeka zaidi pale anapoonekana kuwa anapata mafanikio zaidi na anachukua vikombe ambavyo vinamfanya aonekane bora zaidi.

Kuna watu kama Neymar ambao walikuwa hawatazamiwi kuja iuondoka ndani ya klabu ya Barcelona kwa mazingira ya haraka namna ile lakini jambo lile liliweza kufanyika na liliwezekana kwa nafasi ya pekee sana. Zaidi ya hayo aliondoka katika klabu hiyo akitafuta maslahi zaidi na akaweza kufanikiwa sana kwenye hilo.

Mafanikio ya nyota huyo sio ya kisoka lakini ameweza kuwa ni mtu aliyefanikiwa kutengeneza pesa nyingi sana kwa muda mfupi. Jambo hilo limempa nafasi kubwa na heshima kubwa kwa sababu kwa umri wake na aina ya maisha anayoishi ya kusumbua wawekezaji mbalimbali juu yake ni vitu ambavyo vinampa nafasi ya ubora zaidi.

Ilivyokuwa kwa Koulibaly

Mlinzi wa klabu ya Napoli, Koulibaly amekuwa akihusishwa na kujiunga na klabu ya Manchester United kwa kipindi kirefu sana hadi sasa. Lakini bado uhamisho wake haujaweza kutimia. Jambo hilo linaonekana pia kumuathiri nyota huyo kwa namna moja au nyingine kwa sababu ni kipindi kirefu anatajwa kutaka kujiunga huko.

United ambao wamekuwa na tatizo katika eneo la ulinzi hata baada ya usajili wa nyota wawili Bailly na Lindelof wanekuwa wakimvizia nyota huyo wa Napoli japo majaribio yao yamekuwa yakizuiliwa mara kwa mara kutokana na klabu hiyo kuendelea kuwa na nia ya kumtumia mchezaji huyo.

Nyota huyo anaona kwake Napoli ni zaidi ya nyumbani kwa sababu wengi wameweza kumfahamu zaidi katika safari yake ya soka akiwa Napoli, hivyo anaheshimu uwepo wake hapo na la zaidi anaamini kwamba safari yake ya mafanikio imeweza kupikwa vyema na klabu hiyo. Hivyo, bado hajafanya maamuzi ya kuhama klabuni hapo.

4 Komentara

    Baki tu hapo hapo.

    Jibu

    Baki tu hapo

    Jibu

    Koulibaly beki kitasa

    Jibu

    Koulibaly n mzalendo tosha namkubal sana 👍

    Jibu

Acha ujumbe