Koulibaly: Jackson Anatakiwa Kuwaza Ballon D'or

Beki wa zamani wa klabu ya Chelsea Kalidou Koulibaly amemzungumzia mshambuliaji wa klabu ya Chelsea Nicklas Jackson ambaye ni raia mwenzake wa Senegal na kusema mchezaji huyo anapaswa kuwaza kushinda Ballon D’or.

Koulibaly amesema Jackson anatakiwa kuamini anaweza kua mchezaji wa kiwango cha dunia kwani wachezaji wengi ambao wametwaa tuzo ya Ballon D’or waliamini kua wanaweza kutwaa tuzo hiyo, Hivo amemsihi Nicklas Jackson aamini anaweza kutwaa kua mchezaji bora wa dunia kwakua waliokua waliamini hivo kwanza.koulibaly“Nico Jackson lazima aamini kwamba anaweza kuwa mchezaji wa daraja la dunia. Wachezaji wote waliowahi kushinda Ballon d’Or waliamini kwamba wangeweza. Kwa hivyo, ni lazima kuweka wazo hili kichwani mwa Nico.”

“Simwambii awe mbinafsi na kuwapuuza wachezaji wenzake, lakini ni lazima afikirie kuhusu Ballon d’Or.”

“Ikiwa utaweka picha hii kichwani mwake, anaweza kuifikia. Na hilo ndilo ninamwambia kila mara.”

Beki Koulibaly anaamini mshambuliaji huyo ana ubora ambao unaweza kumfanya akawa mchezaji bora duniani lakini kitu cha kwanza anachotakiwa kukifanya ni kuamini na kuweka kichwani kua anaweza kua mchezaji bora duniani, Mshambuliaji Jackson amekua akirusjiwa maneno na mashabiki wa klabu yake kutokana na kukosa nafasi mara kwa mara lakini anaonekana kuimarika siku baada ya siku.

Acha ujumbe