Mchezaji wa FC Barcelona Jules Kounde pamoja na Maignan wameondolewa kwenye kikosi cha Ufaransa ambacho kinajiandaa na safari yao ya Denmark baada ya kupata majeraha, hali iliyopelekea Didier Deschamps kumuita golikipa Steve Mandanda wa Rennes.

Kounde na Maignan Waongezeka Kwenye Orodha ya Majeruhi

 

Mabao kutoka kwa Kylian Mbappe, na Olivier Giroud yaliihakikishia Ufaransa kupata ushindi wao wa kwanza katika kampeni ya ligi ya Mataifa dhidi ya Austria siku ya Alhamisi, lakini ongezeko la majeraha katika upande wao yanazidi kuogopesha timu ya Ufaransa.

Timu ya Deschamps tayari ilikuwa bila Kareem Benzema, Kingsley Coman, N’golo Kante, Paul Pogba na wengine kwa mechi zao za mwisho kwa ligi ya Mataifa, na Kiungo wa Juventus Pogba hana shaka kushiriki Kombe la Dunia baada ya kufanyiwa upasuaji wa goti.

Les Bleus wanazidi kupungua baada ya beki wa Barcelona Kounde kupata jeraha na kutolewa nje katika dakika ya 23, na sasa imebainika kuwa Maignan alikuwa na maumivu kwenye nyama za paja kabla ya kuondoka kwake kipindi  cha mapumziko.

 

Kounde na Maignan Waongezeka Kwenye Orodha ya Majeruhi

Kipa huyo wa AC Milan Maignan hataweza kucheza, hivyo nafasi yake itachukuliwa na Steve Mandanda ambae ameitwa na Deschamps.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa