Meneja wa Chelsea, Thomas Tuchel amedhibitisha kumkosa kiungo wake Mateo Kovacic ambaye alipata maumivu ya misuli ya paja mwezi uliopita.

Kovacic amekosa michezo minne kwa Chelsea mpaka sasa ikiwemo michezo miwili ya Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya dhidi ya waajiri wake wa zamani, Real Madrid.

 

kovacic, Kovacic Kuwakosa Manchester City Leo., Meridianbet

Tuchel amedhibitisha hayo katika mkutano na waandishi wa habari huku wachezaji wengine wote wakiwa tayari kuwavaa The Citizen.

“Kuhusu majeruhi hakuna kilichobadilika sana” alianza Tuchel

“Bado tunaendelea na mazoezi baadae leo [jana] kama kuna kitu kitabadilika lakini kwasasa kila mchezaji yupo tayari ukimuondoa Kova.

“Bahati mbaya Kova atakuwa nje. Tunatarajia atarudi katika mchezo dhidi ya Arsenal na Wembley katika fainali ya FA dhidi ya Leicester City.

“Itakuwa mchezo dhidi ya Arsenal lakini kwa kesho atakosekana. Kila mchezaji mwingine yupo tayari kwaajili ya mchezo wa kesho.” aliongeza


TENGENEZA FAIDA KUPITIA MCHEZO WA TITAN DICE UKIWA NA MERIDIANBET KASINO

Unapokuwa kwenye Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet, huna sababu ya kucheza kwa mashaka. Titan Dice, ni mchezo unaweza kukupatia mamilioni kwa mzunguko mmoja!

kovacic, Kovacic Kuwakosa Manchester City Leo., Meridianbet

SOMA ZAIDI

7 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa