Kroos Hajui Mustakabali Wake

Kiungo wa klabu ya Real Madrid na timu ya taifa ya Ujerumani Toni Kroos ameweka wazi bado hajajua mustakabali wake kwenye timu ya taifa ya Ujerumani baada ya michuano ya Euro 2024.

Kiungo Toni Kroos ameyasema hayo baada ya kuulizwa swali na waandishi wa habari kama ataendelea kuitumikia timu ya taifa ya Ujerumani baada ya michuano ya Euro 2024 kumalizika.kroosKiungo huyo amesema “Mambo mengi hayako sawa juu ya nini kitatokea baada ya michuano ya Euro,Sijaongezewa hata mkataba mpya na klabu yangu jambo ambalo nataka kumalizana nalo kwanza”

Inafahamika kiungo Toni Kroos amerejea kwenye timu ya taifa ya Ujerumani baada ya kutangaza kuachana na kikosi hicho baada ya michuano ya Euro 2021, Lakini mwaka huu mwezi uliopita alitangaza kurejea kukipiga kwenye timu hiyo.kroosTaarifa zinaeleza kiungo huyo aliombwa na shirikisho la soka nchini humo kurejea kuitumikia timu hiyo baada ya kuonekana bado ana uwezo wa kuendelea kuitumikia timu hiyo, Lakini kiungo huyo inaelezwa anaweza akatangaza kustaafu tena pindi tu michuano hiyo itakapokamilika.

Acha ujumbe