Klabu ya WestHam imefanikiwa kukamilisha usajili wa winga wa kimataifa wa Ghana anayekipiga klabu ya Ajax ya nchini Uholanzi Mohammed Kudus kwa kiasi cha Euro milioni 45.
Westham inaendelea kuongeza nguvu kwenye kikosi chake licha ya kua timu ambayo ilichelewa kufanya usajili zaidi, Lakini mpaka sasa inaonekana kufanya sajili nzuri baada ya kukamilisha usajili wa mchezaji Mohammed Kudus kutoka Ajax.Mchezaji Mohammed Kudus anakwenda West Ham licha ya kuhusishwa na vilabu kadhaa kutoka nchini Uingereza ikiwemo klabu ya Brighton Hove and Albion lakini wagonga nyundo hao kutoka London ndio wamefanikiwa kupata saini ya mchezaji huyo.
Klabu ya Westham chini ya kocha David Moyes msimu uliomalizika uliisha kwa mafanikio makubwa ambapo walifanikiwa kutwaa ubingwa wa kombe la Uefa Conference League, Hivo wanahitaji kuendelea walipoishia kwa msimu huu na ndio maana wanafanya sajili kama za kina Kudus ndani ya timu hiyo.