Kulusevski Amwaga Wino Juventus

Mambo yanaendelea kunoga tukiwa katika mwanzo kabisa wa mwaka! Vinara wa Ligi ya Italia Serie A wamekamilisha usajili wa nyota kutoka Atalanta Dejan Kulusevski.

Nyota huyu mwenye uraia wa Sweden amesaini mkataba wa miaka minne na nusu kwa dau la kuanzia la paundi milioni 35.

Staa huyu ambaye sasa anamilikiwa na Juventus ameruhusiwa kusalia kwa mkopo pale Parma. Kulusevski amefanya vyema na kuvutia macho ya klabu kadhaa zilizokuwa zikimuwinda.

Kinda huyu mwenye miaka 19 tu amefunga magoli 4 na kutoa asisti 7 katika gemu 17 alizocheza za ligi, atasalia kwenye klabu aliyopo hadi mwisho wa msimu huu.

Hata hivyo, wataalamu wa mambo wanateta kuwa kufika kwa Kulusevski kunaweza kumfungulia mialango Emre Can ya kuondoka klabuni hapo.

3 Komentara

    Safi

    Jibu

    Hata hivyo, wataalamu wa mambo wanateta kuwa kufika kwa Kulusevski kunaweza kumfungulia mialango Emre Can ya kuondoka klabuni hapo.

    Jibu

    Hongera kwake

    Jibu

Acha ujumbe