Kumi wa Msimu wa 2018/19

Kama ilivyo kawaida unapomalizika msimu wa ligi lazima kuna nyota ambao huweza kuonekana kuwa wamefanya vizuri zaidi kwenye mchezo fulani ndani ya msimu huo. Hii huweza kuhusisha ligi zote kubwa zinazofahamika Ulaya na zenye majina makubwa kiushindani kutokana na vile kila mmoja alivyo na nafasi yake.

Kwa miaka mingi bado utawala wa Messi na Ronaldo haujawahi kupungua hiyo ikiwa ni pamoja na ubora wao wakati wote na kutokubweteka wakiwa uwanjani kwenye majukumu yao ya timu. Jambo hilo limeendelea kuwa chachu kubwa sana kwao. Baadhi ya nyota ambao wamekuwa katika ubora ndani ya msimu huu ni kama vile:

Cristiano Ronaldo, baada ya kuhamia Serie A bado ameweza kuendelea na utawala wake mzito wa kufumania nyavu pamoja na umri wake kusogea, hicho hakijawa kitisho kwake na ameendelea kudhihirisha hilo kwa kusaidia kuipa Juventus ubingwa mwingine wa ligi yao hiyo; mbali na kushindwa kufurukuta kwenye klabu bingwa.

Lionel Messi, ni miongoni mwa nyota ambao kwa hakika uwezo wao sio wa kubezwa na ana kipaji haswa hata akiwa uwanjani ni tishio kubwa sana kwa timu pinzani. Ni aina ya wachezaji wenye uwezo wa kubadili matokeo wakati wowote. Ameweza kupenya katika nafasi hii mbali na kuwa hajaweza kufanya vizuri kwenye michuano ya klabu bingwa.

Mohammad Salah, wengi waliwahi kufikiri kiwango chake anabahatisha tu na kingekuwa ndani ya msimu mmoja pekee lakini amebadili imani hiyo kwa kuwa na msimu mwingine mzuri mara baada ya kuifikisha klabu hiyo kwenye michuano ya klabu bingwa na hata kutwaa kiatu cha ufungaji bora kwa awamu nyingine.

Kylian Mbappe, nyota huyo wa PSG hajawa tu na nafasi ya kufanya vizuri kwenye michuano ya klabu bingwa lakini amekuwa na upekee sana akiwa uwanjani kwa kuwa mwiba kwa kila klabu anayokutana nayo jambo ambalo kwa uhalisia ni lenye nguvu sana kwake na kwa umri wake ana makubwa zaidi ya kufanya zaidi ya alipo sasa.

Sergio Aguero, mfungaji wa muda wote wa klabu ya Manchester City ambaye ameweza kufanya makubwa sana msimu huu. Ameivusha klabu hiyo katika hatua ambazo zilikuwa ngumu sana na kuweza kupoteza mechi zile ilikuwa ni dalili ya wao kupoteza ubingwa wao. Japo hawajafanya vizuri kwenye klabu bingwa lakini bado wameonesha soka safi sana.

Pamoja na hao kuna wengine pia ambao wameweza kuwa na msimu wenye thamani sana wakiwemo Karim Benzema wa Real Madrid; Timo Werner wa RB Leipzig; Raheem Sterling wa Manchester City; Eden Hazard wa Chelsea; na Edinson Cavani wa Paris Saint-Germain.

3 Komentara

    Safi sana

    Jibu

    Habar njema

    Jibu

    Habar njema

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.