Umeshawahi kufikiri kwa nini ndondi zinapigwa kwa raundi 12? soma stori ya bondia huyu.
Iko hivi, kabla ya mwaka 1982 mapambano yote ya ngumi za kulipwa yilikuwa yanahusisha raundi 15 kwa maana pambano moja lilikuwa linahusisha dakika 45. Tofauti na sasa ambapo raundi ni 12 huku huku pambano zima ikihusisha dakika 36.
Novemba 13, 1982, Kim Duk-koo alikuwa anapigana dhidi ya Ray Mancini nchini marekani pambano ambalo lilikuwa linahusisha raundi 15 na kwa bahati mbaya hii ilikuwa ni mara ya kwanza Kim anacheza pambano la raundi 15 tofauti na Mancini ambaye alikuwa ameshacheza mapambano kadhha ya urefu huo.
Mbali na Kim kuanza vizuri lakini kadiri pambano lilivyozidi kwenda mbele ndivyo ambavyo hali ilizidi kuwa mbaya kwa Kim ambapo ilipofika raundi ya 14 aliruhusu ngumi nyingi ambazo zilimfanya aweze kudondoshwa na hivyo kupoteza kwa TKO na badae kupoteza fahamu. Na siku chache badae akafariki akiwa COMA.
Kifo cha Kim kilipelekea Mama yake mzazi kujiua kwa msongo wa mawazo na badae mwamuzi ambaye alichezesha pambano la Richard Green naye akajiua kwa kujihisi kuwa na hatia kwa upotevu wa maisha ya bondia Kim. Baada ya hiki kifo cha Kim ndo mamlaka mbalimbali za ndondi nchini marekani wakafanya marekebisho kadhaa kwenye kanuni za mchezo.
Ambapo mwaka 1982, WBC ndo ilikuwa chombo cha kwanza kupitisha marekebisho ya kupunguzwa kwa raundi za mchezo kutoka 15-12 ambazo zinatumika mpaka sasa. Na baadae taasisi nyingine kama IBF, WBA na WBO nao wakafuata hayo maamuzi ya kupunguza urefu wa pambano kwenye ngumi za kulipwa.
Una Kila sababu ya kufurahia wiki yako na kutengeneza mwaka huu uwe wa faida zaidi katika kasino zetu za mtandaoni za meridianbettz. Mchezo wa Zeus Ancient Fortunes unakuongoza kutekeleza hilo.