Soka ni mchezo ambao huwa na muunganiko wa mambo mengi sana ambayo huibua hisia za aina tofauti, kuchochea furaha kuliko ilivyo kawaida na hata kuongeza hamasa kwa washindani pale wanapotengeneza historia ndani yake. Mbali na hilo soka ni mchezo wa makosa ambapo bila hilo hakuna ambaye angefurahia mchezo huu.

Luis Figo ni kati ya watu wakubwa kuwahi kucheza soka katika ligi ya Hispania hususan klabu ya Real Madrid ambako aliweka historia ya aina yake ndani ya klabu hiyo na hata ligi ya nchini humo kutokana na uwezo wake mkubwa wa kuuchezea mpira na hata uwezo wake wa pekee katika kikosi hicho.

Mashabiki ambao mara nyingi ndiyo tunaowaita wachezaji namba 12 waliopo uwanjani wanaweza aidha kumpa nguvu mchezaji au kumuondoa mchezoni, walikuwa na nafasi kubwa sana kwenye maisha ya nyota huyo hasa katika nafasi ya kumjenga kutokana na mgandamizo waliokuwa wakimpa nyota huyo akiwa uwanjani.

Nyota huyo anasema mechi zao za El Classico ndizo ambazo zilikuwa zikimpa ari kubwa sana ya kupambana uwanjani kutokana na kile mashabiki zao walikuwa wakikitaka. Furaha ya mashabiki ni furaha ya wachezaji pia, kwa hiyo bila mashabiki wao hawakuwa na nafasi ya kufanya maajabu yoyote yale.

Kilichomfanya nyota huyo azomewe na kutukanwa sana ndani ya mkutano wa wawili hao ni hatua yake ya kuwahama Barcelona na kujiunga na Madrid ambao ni mahasimu wa kisoka katika uhamisho ambao ulikuwa na utata na ulikuwa na rekodi katika wakati ule. Uhamisho wake uligharimu £62m hivyo akawa kama adui wa mashabiki hao.

Kwake vitisho, matusi na kuzomewa kulimpa umaarufu mkubwa sana ndani ya soka na kutokana na uwezo wake hakubweteka, alijitahidi kupambana ili kuutumia vyema umaarufu anaotengenezewa na alifanikiwa kwa asilimia kubwa kwani anasema alipokea madili mengi kupitia hilo.

Alichokuwa akikiamini yeye ni kupambana zaidi kupitia ile picha ambayo mashabiki wa pande zote mbili wamewekeza juu yake. Anasema alikuwa anapata wakati mgumu sana anaporudi kucheza Catalunya kutokana na aina ya mashabiki ambao alikuwa anakutana nao ndani ya uwanja huo na hasira walizokuwa nazo juu yake.

2 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa