Klabu ya Man United wanaripotiwa kuwa waliamua kutemana na dili la kumsajili nyota Gareth Bale kwenye usajili wa msimu wa joto kwa sababu ya shida ya majeraha.

Kwa mujibu wa wa Daily Mirror, Mashetani wekundu walikuwa tayari kumsajili nyota huyu kwa mkopo kwa msimu wa 2018/19.

Hata hivyo Man United wakaamua kusitisha mpango wa kumsajili kwa sababu ya ripoti kuwa asingweza kumaliza msimu mzima kwa sababu ya rekodi yake ya majeraha.

Hata hivyo, taarifa zinataja kuwa Klabu hii haikupendezwa kuanza kumlipa bale mshahara wa paundi laki tano kwa kiki wakati angeweza kucheza sehemu tu ya msimu na sio msimu wote.

Mashetani wekundu hawaonekani kama wanaweza kurejea maamuzi yao ya kumsajili Bale ambaye Zidane alisha mwambia kuwa yeye ni ziada kwa kikosi chake cha Real Madrid.

2 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa