Kyle Walker Raha tu Ndani ya Man City

Beki wa klabu ya Manchester City na timu ya taifa ya Uingereza Kyle Walker anafurahia maisha tu ndani ya klabu ya hiyo baada ya kujiunga kutoka klabu yake ya zamani ya Tottenham Hotspurs.

Kyle Walker amefanikiwa kua na mafanikio makubwa baada ya kujiunga na klabu ya Manchester City mwaka 2017 chini ya kocha Pep Guardiola, Kwani beki huyo wa kimataifa wa Uingereza alijiunga na City akiwa na miaka 27 mwaka 2017 akiwa hajashinda taji lolote lakini mpaka sasa ana mataji 13 ndani ya Man City akiwa na umri wa miaka 33.Kyle WalkerKupitia beki huyo na mifano mingi ya wachezaji wengine inaendelea kuonesha namna gani klabu ya Tottenham ina changamoto kwa upande wa kutwaa mataji na kama mchezaji anahitaji mafanikio zaidi anapaswa kuondoka klabuni hapo, Kupitia kigezo hicho mshambuliaji Harry Kane anazungumzwa zaidi kutaka kuondoka ndani ya timu hiyo kutokana na hali ambayo inaendelea ndani ya timu hiyo.

Beki Kyle Walker ameshafanikiwa kushinda mataji kumi na tatu mpaka sasa ndani ya Manchester City tangu aondoke Tottenham miongoni mwa mataji hayo ni pamoja na mataji matano ya ligi kuu ya Uingereza, Mataji manne ya kombe la ligi, pamoja na mataji mawili ya kombe la FA Cup.Kyle WalkerLicha ya kushinda mataji na klabu ya Manchester City beki Kyle Walker amekua moja ya mchezaji muhimu kwenye kikosi cha kocha Pep Guardiola kwa kipindi chote cha mafanikio ambacho amekua nacho klabuni hapo,Beki huyo wa kimataifa wa Uingereza bado anasalia kua muhimu kwenye kikosi hicho licha ya majeraha ambayo yamekua yakimuandama mara kwa mara kwasasa.

Acha ujumbe