Nyota wa PSG, Kylian Mbappe amebainisha kuwa bado hajafanya maamuzi juu ya hatma yake, lakini ni vitu vichache tu vimesalia kwake kuamua.

Nyota huyu ambaye amekuwa akifanya vyema kwenye League 1, akifanikiwa kuwa mchezaji bora maratatu mfululizo hadi msimu huu, anatarajiwa kutawala vichwa vya habari za michezo kwa wiki kadhaa zijazo.

Tetesi zinazopewa uzito zaidi ni kuwa staa huyu yuko mbioni kujiunga na klabu ya Real Madrid msimu huu wa joto.

Kwa mujibu wa Goal, wakimnukuu Kylian Mbappe, wanasema kuwa “Jambo limeisha, vimebaki vitu vichache tu” kufanya maamuzi.

Hata hivyo, kuna taarifa kuwa staa huyu bado hana uhakika kuhusu klabu ambayo anaenda kuichezea msimu ujao, vilabu kadhaa vikitarajiwa kugongana sokoni kwa saini yake.

Mbappe amekuwa mchezaji bora kwa mara ya tatu mfululizo akiwa na magoli 25 ya ligi, na asisti 17″

Kylian Mbappe
Kylian Mbappe

“Mchezaji bora wa Ligue 1 kwa msimu wa tatu mfululizo. Ni heshima kubwa kuandika historia hii tena. Hii inaufurahisha moyo wangu. Naishukuru klabu yangu, wote na mashabiki kwa uaminifu nilioupata msimu huu.”


 

 


TENGENEZA FAIDA NA ZEUS ANCIENT FORTUNES

Una Kila sababu ya kufurahia wiki yako na kutengeneza mwaka huu uwe wa faida zaidi katika kasino zetu za mtandaoni za meridianbettz. Mchezo wa Zeus Ancient Fortunes unakuongoza kutekeleza hilo.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa