Safari ya Antoine Griezmann kutua Barcelona inaweza kukutana na kikwazo. Uongozi wa La Liga, kupitia raisi wake Javier Tebas umezungumzia suala la uhamisho wa staa huyu kuingia Barcelona.

Atletico Madrid wanaripotiwa kulalamika kulikuwa na kasoro fulani Barcelona wakiweka kitita cha euro milioni 120 kwa ajili ya kumnasa staa huyu kwa dau la kununua mkataba wake, Barcelona wanalalamikiwa kutangaza kumnunua Griezmann.

Dau la kumnasa staa ghuyu lilishuka kutoka euro milioni 200 hadi kufikia euro milioni 120. Julai 1. Hata hivyo, Atletico wanalalamikia kuwa dili la uhamisho wa staa huyo lilifanyika mapema zaidi hivyo Barcelona wanahitajika kulipa zaidi.

“Inawezekana kuzuia uhamisho wa mchezaji. La Liga wanatakiwa kuamua ni uamzi upi wachukue.”

Griezmann tayari ameshaanza kukipiga na Barcelona akiwa amecheza mechi ya kirafiki na klabu yake mpya walipochapwa 3-1.

Uongozi wa La Liga unadai kuwa kwa sasa jambo hili linafanyiwa uchunguzi baada ya hapo maamuzi yatafanyika mezani. Klabu ya Atletico iliwashtaki Barcelona kwa shirikisho la soka ulimwengungi FIFA kuwa walikiuka taratibu za usajili walipokuwa wakimfukuzia Griezmann mwaka 2017.

ONI MOJA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa